Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-11-25 15:05:35    
Siku ya kimataifa ya kutokomeza vitendo vya kimabavu nyumbani

cri

    Tarehe 25 Novemba ya kila mwaka ni siku ya kutokomeza vitendo vya kimabavu nyumbani kwa watu. Hii iliamuliwa tarehe 3 Novemba mwaka 1999 kwenye Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kutokana na pendekezo la Jamhuri ya Dominica.

    Vitendo vya kimabavu nyumbani kwa watu vinafuatiliwa na kuzingatiwa siku hadi siku na nchi mbalimbali duniani. Mwezi Julai mwaka 1981, mkutano wa kwanza wa wanaotetea haki za kina mama wa Latin Amerika ulitangaza kuwa tarehe 25 Novemba kuwa siku ya kupinga vitendo vya kimabavu, ili kuwakumbuka wanawake watatu wa Dominica?kinadada watatu wa familia ya Milaber ambao waliuawa na madikteta tarehe 25 Novemba mwaka 1960. Mkutano huo pia uliamua kuwa kila mwaka zifanyike shughuli za uelimishaji kwa siku 16 mfululizo kuanzia tarehe 25 Novemba hadi tarehe 10 Desemba.

    Tarehe 25 Novemba mwaka 1993, Umoja wa Mataifa ulitoa "Taarifa ya kutokomeza vitendo vya kimabavu dhidi ya kina mama", ambayo ilithibitisha maana ya vitendo vya kimabavu dhidi ya kina mama, yaani ni vitendo vyote vya kijinsia vilivyosababisha au vitakavyoweza kusababisha madhara na uchungu kwa rohoni mwa watu au katika vitendo vya kujamiiana.

    Tarehe 8 Mwezi Machi mwaka 1999, Shirika la fedha la kina mama la Umoja wa Mataifa liliitisha mkutano wa dunia nzima kupitia njia ya televisheni kwenye Baraza kuu la Umoja wa Mataifa, kauli mbiu ya mkutano huo ilikuwa ya kupinga vitendo vya kimabavu nyumbani kwa watu, ambapo shirika hilo lilianzisha shughuli nyingi za kueneza ujuzi kuhusu kutokomeza vitendo vya kimabavu dhidi ya kina mama katika sehemu ya Afrika na Pasifiki, Latin Amerika na Caribbean.

    Uchunguzi husika ulionesha kuwa, kote duniani kina mama wasiopungua theluthi moja waliwahi kupatwa na vitendo vya kimabavu, unyanyasaji wa kingono au unyanyasaji wa aina mbalimbali katika maisha yao yote, na watu wengi waliofanya vitendo vya kimabavu walikuwa watu wa familia zao. Vitendo vya kimabavu nyumbani kwa watu ni uvamizi dhidi ya haki na uhuru wa kimsingi wa kina mama, ambavyo si kama tu vinaweza kusababisha kuvunjika kwa ndoa na kusambaratika kwa familia, bali pia vinadhuru vibaya roho na afya za wanawake. Kama vitendo vya kimabavu nyumbani kwa watu havitaweza kudhibitiwa au kuzuiliwa kwa wakati na kwa mafanikio, vitendo hivyo huwa vinaweza kuongezeka na kuwa matukio mabaya, na kusababisha mikwaruzano mibaya ya kiraia au kesi nyingi za jinai, ambazo zinaathiri vibaya utulivu na usalama wa jamii.

    Wataalamu wanaona kuwa, vitendo vya kimabavu nyumbani kwa watu hutokea ndani ya familia, hivyo madhara yake na ubaya wake huwa haviwezi kuzingatiwa ipasavyo. Kutokomeza vitendo vya kimabavu nyumbani kwa watu kunatakiwa kufuatiliwa na jamii nzima na kufanya juhudi za pamoja, huu ni wajibu ambao kila nchi inapaswa kuubeba. Wataalamu hao wanazitaka serikali za nchi mbalimbali zifuate ahadi zao kwa vitendo, kufanya ushirikiano na vikundi vya jamii, watu wanaotetea ulinzi wa haki za binadamu na wataalamu wanaohusika, ili kutoa ulinzi na misaada kwa watu waliodhuriwa, na kuimarisha elimu husika ili kulinda haki na maslahi ya kina mama kupitia taratibu mbalimbali.

Idhaa ya Kiswahili 2004-11-25