Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-11-25 19:28:57    
Wakazi wa Beijing wafuatilia ununuzi wa vitu visivyo na uchafuzi

cri

    Katika miaka ya hivi karibuni, wakazi wa Beijing wanafuatilia sana kununua vitu visivyo na uchafuzi. Wanaponunua bidhaa za elektroniki huzingatia sifa yake ya kuokoa nishati, wanaponunua mboga na vyakula huchagua vile visivyochafuliwa, na wanapopamba nyumba zao hawawezi kusahau hununua vifaa visivyokuwa na uchafuzi kwa afya.

    Bwana Liu Mingyin anafanya mapambo kwa nyumba yake. Kwa kuwa ana mtoto mwenye umri wa miaka miwili, hivyo anafuatilia sana kama vifaa anavyotumia vina uchafuzi au la. Alisema:

    "Mtoto huwa ni mtundu, atatafuna meza na viti, hata atainamia kuramba sakafu, hivyo wakati wa kupamba nyumba bora kutumia vifaa visivyo na uchafuzi. Mimi natumia sakafu ya mianzi, ambayo haikutumiwa dawa za kemikali wakati wa kutengenezwa, hivyo ni salama. Rangi niliyotumia kupaka ukuta pia hakuna harufu mbaya."

    Kama ilivyo kwa Bwana Liu, hivi sasa wakazi wengi mjini Beijing wanafuatilia kuchagua vifaa visivyo na uchafuzi wakati wa kupamba nyumba zao. Wanaona kuwa, makazi ni mahali muhimu kabisa katika maisha yao, hali ya makazi inahusiana moja kwa moja na hali ya kimaisha. Hivyo wanapopamba nyumba zao hufuatilia kuchagua vifaa visivyo na uchafuzi.

        

    Katika upande wa chakula, wakazi wa Beijing si kama tu wanafuatilia virutubisho vya chakula, bali pia wanafuatilia sana kama chakula kinakuwa na uchafuzi. Kwenye duka kuu la kujihudumia, mwandishi wa habari ameona kuwa, aina nyingi za vyakula kama vile mchele, unga wa ngano, mafuta, mboga na matunda vinabandikwa na kadi maalum yenye ishara ya kutokuwa na uchafuzi. Japokuwa bei za vitu hivyo dukani ni ghali zaidi kuliko vile vinavyouzwa kwenye magulio, lakini wateja wengi wangali nunua kutoka dukani. Bwana Zhang Hongcheng aliyenunua vitu kwenye duka hilo alisema:

    "Japokuwa bei za vyakula visivyo na uchafuzi ni kubwa zaidi kuliko vyakula vya kawaida, lakini napendelea kuchagua vyakula hivyo kutokana na sababu ya afya. Mimi pia najaribu kuwashawishi marafiki zangu kununua vyakula visivyo na uchafuzi, ili kuinua hali yetu ya maisha."

    Baadhi ya wakazi wa Beijing hata wanaonesha mawazo yao ya kutochafusha mazingira katika vitendo vyao vya kila siku. Bibi Ge Lihua ni mfanyakazi mstaafu, zamani alikuwa antumia mfuko wa plastiki kununua mboga, sasa ameacha tabia hiyo, badala yake, alitengeneza mfuko wa kununulia vitu kwa nguo iliyochakaa. Alisema:

    "Mfuko wa plastiki ni kitu kisichoweza kuyeyuka katika ardhi, kitaleta uchafuzi kwa mazingira, mara moja nikinunua aina nyingi za mboga, huwa napewa mifuko mingi ya plastiki. Sasa natumia mfuko wa kudumu nilioutengeneza mwenyewe, mfuko huo hautaleta uchafuzi wowote kwa mazingira."

    Bibi Ge pia amekusanya mifuko zaidi ya 2000 ya plastiki aliyopewa wakati wa kununua vitu kwenye maduka ya kujihudumia na kuikabidhi kwa idara husika. Katika mtaa anaoishi Bibi Ge, wakazi wengine pia wamekuwa na uzoefu huo mzuri, kwa mfano, kila familia inatenganisha takataka, familia nyingi zinatumia taa za kuokoa nishati, na friji isiyotumia freon.

    Zaidi ya hayo, wakazi wa Beijing pia wanafuatilia vitendo vyao visilete uchafuzi kwa mazingira. Wanatupa betri zilizotumika katika sanduku maalum la kurudisha betri hizo, ili kuzizuia zisichafushe mazingira; mikahawa mingi inakusanya vijiti vilivyotumika na kuvikabidhi kwa idara husika kwa matumizi mengine.

    Wataalamu wametathmini sana ueneaji wa matumizi ya vitu visivyo na uchafuzi mjini Beijing. Mkuu wa kituo cha utamaduni wa mazingira cha kijiji cha dunia cha Beijing Bibi Liao Xiaoyi alisema:

    "Mawazo ya matumizi ya vitu visivyo na uchafuzi si kama tu yameonesha kuinuka kwa hali ya maisha yetu, bali pia yameonesha kuinuka kwa mwamko wa wakazi wa kuhifadhi mazingira. Wakazi wamefahamu kuwa, matumizi ya kila siku huambatana na hifadhi ya mazingira. Wakazi wengi wameanza kuelewa kuwa, kila mtu anaweza kujiunga na hifadhi ya mazingira kwa njia yake ya maisha inayosikilizana vizuri na mazingira, si lazima kujiunga moja kwa moja na kazi ya kuhifadhi mazingira."

    Bibi Liao alisema kuwa, hivi sasa idadi ya wakazi wanaofuatilia ununuzi wa vitu visivyo na uchafuzi nchini China imeongezeka siku hadi siku. Jambo la kuwafurahisha watu ni kwamba, vitendo na mawazo ya matumizi ya vitu visivyo na uchafuzi si kama tu vimeenea katika wakazi wa mijini, bali pia vimeonesha katika wakazi wa vijijini, hali hiyo kwa upande mmoja imedhihirisha kuinuka kwa hali ya maisha ya wachina.

Idhaa ya Kiswahili 2004-11-25