"Ripoti ya maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi mwaka 2004" iliyotolewa tarehe 23 na shirika la kupambana na ukimwi la Umoja wa Matifa na shirika la afya duniani inaonyesha kuwa, ingawa kazi ya kinga na tiba ya ugonjwa wa ukimwi duniani imepata maendeleo kwa kiasi fulani katika miaka miwili iliyopita, lakini kutokana na hali ilivyo sasa ya mwelekeo wa maambukizi ya ugonjwa huo, hali ya kinga na tiba yake bado ni ngumu.
Ripoti hiyo inasema kuwa, kazi ya kinga na tiba ya ugonjwa wa ukimwi katika nchi za Afrika ya Mashariki imepata maendeleo makubwa katika miaka kadhaa iliyopita. Kwa mfano idadi ya watu walioambukizwa na virusi vya ukimwi huko Addis Ababa mji mkuu wa Ethiopia imepungua kuwa asilimia 11 katika mwaka 2003 kutoka asilimia 24 katika miaka ya 90 karne iliyopita; na ile ya Kenya imepungua kuwa asilimia 9.4 katika mwaka 2002 kutoka asilimia 13.6 katika mwaka 1997.
Lakini idadi ya watu walioambukizwa virusi vya ukimwi katika dunia nzima imefikia kiwango kipya, na kuvuka milioni 39, na kati ya idadi hiyo watu milioni 49 ni maambukizi mapya, na wagonjwa wengine zaidi ya milioni 3 walikufa mwaka huu.
Sehemu za kusini mwa jangwa la Sahara bado ni sehemu iliyoathiriwa vibaya zaidi na virusi vya ukimwi, idadi ya watu walioambukizwa katika sehemu hiyo ni zaidi ya asilimia 25, hata umri wa wastani wa watu wa nchi 9 za sehemu hiyo ni chini ya ule wa miaka 40 iliyopita; katika sehemu ya bahari ya Carribean, ugonjwa wa ukimwi umekuwa chanzo kikubwa kabisa cha vifo vya watu wenye umri kati ya miaka 15 na miaka 44; huko Amerika ya Kaskazini, idadi ya wanawake wanaoambukizwa inaendelea kuongezeka; na katika sehemu ya Ulaya ya magharibi, idadi ya watu wanaoambukizwa kwa njia ya kujamiiana iliongezeka maradufu kuanzia mwaka 1997 hadi 2002.
Katika sehemu ya Ulaya ya mashariki na Asia ya kati, hali kutumia dawa za kulevya kwa kujidunga sindano inaongezeka kwa kasi, na kusababisha idadi ya watu wanaoambukizwa kuendelea kuongezeka. Katika taarifa iliyotolewa siku hiyo, katibu mkuu mtendaji wa shirika la kupambana na ukimwi la Umoja wa Mataifa Bw. Peter Piot alisema kuwa, "Katika nchi nyingi, tatizo la mashoga na watu wanaotumia dawa za kulevya kwa njia ya kujidunga sindano hayakutiliwa maanani katika kazi ya kinga na tiba ya ugonjwa wa ukimwi, serikali za nchi mbalimbali zinapaswa kutambua suala hilo.
Ripoti hiyo pia ilieleza kuwa, fedha zilizolengwa kwa ajili ya kinga na tiba ya ugonjwa wa ukimwi zimeongezeka na kuwa dola za marekani trilioni 6.1 katika mwaka 2004 kutoka dola za marekani trilioni 2.1 katika mwaka 2001. Uchunguzi kwa nchi 71 zenye mapato wastani na madogo uliofanyika hivi karibuni unaonyesha kuwa, katika miaka 3 iliyopita, idadi ya wanafunzi wa sekondari walioelimishwa kuhusu ugonjwa wa ukimwi iliongezeka maradufu, na huduma ya kinga ya kuzuia virusi vya ugonjwa huo kutoka kwa mama mja mzito kwenda kwa watoto wachanga pia iliongezeka kwa asilimia 70. Lakini, shirika la kupambana na ukimwi la Umoja wa Mataifa lilikisia kuwa, watu milioni 5 hadi 6 duniani wanatarajiwa kupatiwa tiba ya kuzuia kurudia kwa ugonjwa huo, lakini miongoni mwao chini ya asilimia 10 wana uwezo wa kugharamia tiba hiyo.
Ripoti hiyo ilisema kuwa, hivi sasa binadamu bado wako mbali na lengo ambalo wanaweza kudhibiti ugonjwa wa ukimwi, jumuiya ya kiamtaifa na serikali za nchi mbalimbali zinapaswa kuzidisha kazi ya kinga na tiba ya ugonjwa huo.
Idhaa ya Kiswahili 2004-11-26
|