Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-01 18:33:17    
Kofia za Watoto

cri

    Kupata watoto ni jambo la furaha kwa familia. Katika Jimbo la Shanxi, watu hufanya sherehe mbalimbali za kutoa pongezi siku mtoto anapozaliwa, kutimiza mwezi mmoja, siku mia na mwaka mmoja. Zawadi muhimu katika sherehe hizo ni kofia zenye rangi za kupendeza, hii ni mila ya watu wa huko.

    Aina za kofia za watoto huwa za mitindo tofauti na hutengenezwa ili ziendane na mabadiliko ya hali ya hewa. Watoto wanavaa kofia zilizojazwa pamba wakati wa majira ya baridi na kofia zenye matabaka mawili wakati wa majira ya kuchipua na mpukutiko. Maumbo ya kofia ni ya namna tofauti na ya kuvutia, kofia za watoto wa kiume zina maumbo ya simba, kichwa cha chui, kichwa cha joka na kofia za wasichana zina maumbo ya sungura, samaki wa dhahabu na mayungiyungi.

    Kutokana na kuabudu wanyama, itikadi za kijadi zinasema kwamba wanyama wanaoashiria baraka kama vile simba na chui wanaweza kutoa sadaka, kuomba mungu na kuhifadhi watoto, kuleta baraka na kuondoa msiba, hizo ndiyo sababu kofia za aina hizo zinapendwa zaidi.

    Kina mama ni hodari wa kufuma kofia nzuri za kutunza joto. Kutokana na ujuzi wao mwingi wa maisha na mapenzi kwa watoto, wanaweza kufuma kiustadi kofia zenye manufaa mengi. Sehemu ya mbele ya kofia hushonwa kwa matabaka kadha ili iwe na umaalumu kama dereya, zinaonekana imara na pia zinaweza kuzuia nguvu ya upepo. Mkia wa kofia unashonwa kwa vipande viwili kama mkia wa samaki na kufunika shingo. Ubavuni mwa kofia huning'inia tepe mbili zinazoweza kufungiwa kidevuni ili kofia zisianguke na ili iwe rahisi kuishika mkononi. Kwenye ncha ya mkia hushonewa kengele mbili zinazoweza kulia.

    Kofia tunazozitaja hapa ni hifadhi ya nusu karne iliyopita, lakini mila ya kushona kofia bado inaendelezwa mpaka leo.

Idhaa ya Kiswahili 2004-12-01