Shirika la afya duniani WHO jana lilitoa taarifa kabla ya siku ya 17 ya UKIMWI duniani ikizitaka nchi mbalimbali zichukue hatua halisi za kuhakikisha wagonjwa wanawake wa UKIMWI wanapewa kwa usawa tiba ya kuzuia ugonjwa wa UKIMWI.
WHO imeainisha kuwa mpaka hivi sasa asilimia 47 ya wagonjwa wa UKIMWI duniani ni wanawake, lakini wamekumbana na matatizo wakati wa kupatiwa matibabu na nchi mbalimbali zinatakiwa kuwapatia huduma mbalimbali.
Rais Yoweri Museveni wa Uganda tarehe 29 alitangaza kuwa idadi ya watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI nchini Uganda imepungua kuwa asilimia 6 kutoka asilimia 18 ya miaka ya 90 ya karne iliyopita. Jambo hilo linaonesha kuwa ugonjwa wa UKIMWI umedhibitiwa katika nchi hiyo baada ya kufanya jitihada kwa zaidi ya miaka 10.
Leo ni siku ya ugonjwa wa UKIMWI duniani na kauli mbiu ya mwaka huu ni "kuwatunza wanawake na kupambana na UKIMWI".
|