Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-02 20:56:58    
Hongkong yafanya shughuli mbalimbali kuiadhimisha siku ya ugonjwa wa Ukimwi duniani

cri

    Tarehe mosi Desemba ilikuwa ni siku ya ugonjwa wa Ukimwi duniani. Huko Hongkong watu kutoka sekta mbalimbali walivaa alama ya tepe nyekundu kifuani, na kuonesha upendo kwa wagonjwa wa Ukimwi kwa njia tofauti.

    Mgonjwa wa kwanza wa UKIMWI aligunduliwa mara ya kwanza huko Hongkong mwaka 1988. Jana, Maonesho makubwa ya matangazo na nyaraka za habari yaitwayo "miaka 20 ya Ugonjwa wa Ukimwi katika Hongkong" yalifanyika katika kituo cha utepe mwekundu cha Hongkong, ili kuinua kiwango cha ufuatiliaji wa wakazi kwa ugonjwa huo na kuwahamasisha wakazi wa Hongkong kuwaunga mkono zaidi wagonjwa wa Ukimwi.

    Kamati ya mfuko wa Ukimwi ya Hongkong na kituo cha mafunzo ya Ukimwi kwa vijana cha Hongkong zilifanya tamasha katika mwangaza wa mishumaa kwenye sehemu tofauti. Kupitia muziki, michezo ya kuigiza na dansi, watu wanaojitolea kutoka kwenye jumuiya hizo mbili walieneza moyo wa kuwafuatilia wagonjwa wa Ukimwi na kuwahamasisha wakazi wa Hongkong kushirikiana katika kupambana na kukinga ugonjwa huo.