Sanamu za ukutani zenye sura za wachezaji wa opera za mitindo ya aina kwa aina na zenye kuonyesha uhai zimetengenezwa kwa makopo yaliyotupwa au vizibo vya chupa za divai, na zinawastaajabisha sana watu. Sanamu hizi ni kazi ya mikono ya Lu Rongwei, kada wa Idara ya Sanaa na Michezo ya Eneo la Huangpu, mjini Shanghai.
Mara baada ya Lu Rongwei kuona sanamu ya mtu iliyofinyangwa na kupakwa rangi nyeusi alikata shauri kujaribu kutengeneza sanamu za wachezaji wa opera kwa kutumia makopo yaliyotupwa. Alitumia vizuri rangi mbalimbali za nje ya makopo na sehemu ya ndani ya makopo yenye kung'ara kama kioo na maarifa yake ya kisanaa kutengeneza aina za sanamu za ukutani zenye sura za wachezaji wa opera walioonekana kuwa hai. Katika uvumbuzi wake alitumia ufundi wa kuchora michoro na maarifa mingi ya miaka mingi ya kufahamu sana maumbo mengi ya opera mbalimbali ili kutengeneza sanamu hizi. Alichunguza kwa makini enzi na umri wa wachezaji wa opera ili kuzidisha matokeo mazuri ya sanaa. Katika utengenezaji wake, alitumia njia za kukunja, kukatakata, kuviringa, kuchonga, kuunganisha na kutundika ukutani ili kila nnjia isaidie kutoa mlingano wa tabia za wachezaji na hali ya nje ya sura zao. Katika vitu alivyotumia llicha ya makopo na vizibo vya chupa za divai, anatumia kokwa za zeituni, pini za ofisini, vibanio na pini za ukutani.
Katika muda wa miaka mitano tangu alipoanza kutengeneza sanamu ya kwanza ya mchezaji wa opera hadi leo, amefanikiwa kutengeneza sanamu zaidi ya 100. Kila sanamu inaonyesha ufundi wa pekee na uzuri maalumu unaowapendeza watu. Alipanga mpango wa miaka miwili mfululizo kumaliza utengenezaji wa sanamu 300 za wachezaji wa opera.
Idhaa ya Kiswahili 2004-12-03
|