Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-06 19:30:36    
Tembea peponi mwa dunia

cri

Sehemu ya Jiuzhaigou ni bonde la mlima lenye urefu wa zaidi ya kilomita 40, jina lake Jiuzhai linatokana na vijiji 9 vya kabila la watibet, eneo la sehemu hiyo ni kilomita 620 za mraba. Kwenye bonde la Jiuzhaiguo, kuna watu wachache, mandhari ya kimaumbile ya huko bado ni ya kiasili. Ukiingia ndani ya bonde hilo, utaona mandhari ya sehemu hiyo ni ya kupendeza sana, milima ya kijani, maji ya mto tulivu, madaraja marefu ya kamba yanayoyumbayumba, mawingu yanayoelea milimani, hasa maji ya mto yanayoweza kubadilika rangi kila mara, ambayo yanaonekana ya rangi ya buluu mithili ya jade ya buluu. Wakati mwingine maji hayo huonekana ya kijani, na wakati fulani maji hayo yanachanganyika na rangi ya kimanjano. Mtalii mmoja kutoka Canada alisimulia jinsi alivyoyaona maji ya Jiuzhaiguo, akisema:

    Naitwa Linda, natoka Canada. Sehemu ya Jiuzhaiguo ni yenye mandhari nzuri kabisa. Hasa maji ya sehemu hiyo, sijui kwa nini maji ya hapa ni ya buluu namna hii, hata zaidi kuliko rangi ya buluu ya anga. Sehemu ya Jiuzhaiguo kweli ni sehemu inapendeza sana, na hata ni nadra kupatikana hapa dunia.

    Maji yenye rangi mbalimbali yanatiririka kwa utulivu kwenye bonde, wakati fulani yanaonekana kama ukanda mrefu mwembamba unaoning'inia milimani; baada ya muda unaweza kuona maji ya mto yanapitapita ndani ya misitu, na kuwa kama maziwa masafi ya uwanda wa juu; na baadaye unaweza kuona kuwa maji ya ziwa yanakuwa maporomoko mbalimbali yanayoanguka kwa kasi ndani ya misitu. Maporomoko hayo pia yanaonekana kwa sura mbalimbali. Baadhi yake yanaingia chini ya bonde, na milio yao ni kama radi, na yanaweza kwenda kasi na mawimbi mengi; baadhi yake yanaporomoka kwa utulivu kama yalivyo mawingu ya angani, yanaingia ndani ya maziwa. Yanayoshanga watu zaidi ni maporomoko yale ya ngazi mbalimbali ambayo yanafuata mwelekeo wa mlima yanaporomoka moja baada ya lingine ndani ya misitu, na kuingia ziwani kwa utaratibu kama hariri ilivyo. Maporomoko hayo ya ngazi mbalimbali yanapendekeza sana kiasi cha kusisimua watu.

    Bwana Zhou Shigang mwenye umri wa miaka zaidi ya 50 ni mtalii kutoka Chongqing, kusini magharibi ya China. Alipotembelea sehemu ya Jiuzhaiguo, alitembea kwa miguu bila kupumzika kwa zaidi ya kilomita 10, hata hakujisikia uchovu. Alisema kuwa, maji ya maziwa ya Jiuzhaiguo yana rangi nzuri sana, hata yanawafanya watu kusahau uchovu:

    Bwana Zhou alisema, maji ya maziwa ya Jiuzhaiguo yana rangi nzuri kabisa, ambayo ni safi sana, rangi yake mbalimbali yana mvuto mkubwa . Hasa maziwa mengi ya sehemu hiyo, maji yake ni ya rangi ya buluu kabisa ambayo inawapendeza watu sana.

    Bwana Zhou alipotaja maziwa hayo aliyaita kuwa ni Haizi, maana yake ya kichina ni "watoto wa bahari", Haizi ni jina maalum la maziwa makubwa na madogo zaidi ya 100 ya bonde la Jiuzhaiguo lililotolewa na watu wa kabila la Tibet wanaoishi huko. Watibet wanaoishi kwenye uwanda wa juu wengi hawajawahi kuona bahari, ndiyo maana waliyaita maziwa ya milimani mbele ya nyumbani kwao kuwa ni "Haizi" yaani "watoto wa bahari. Maziwa hayo yenye rangi mbalimbali yametapakaa kwenye sehemu ya Jiuzhaiguo, na yanabadilikabadilika rangi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na majira, kuwafanya watu waishi katika dunia inayosimuliwa katika hadithi.

Idhaa ya kiswahili 2004-12-06