Wataalamu wa idadi ya watu duniani wanaohudhuria mkutano wa wakuu kuhusu familia duniani wa mwaka 2004 hapa Beijing wanaona kuwa, China ikiwa nchi yenye idadi kubwa zaidi na familia nyingi zaidi kuliko nchi nyingine duniani, imepata mafanikio yanayofurahisha katika kusukuma mbele maendeleo ya uwiano ya idadi ya watu na jamii, lakini bado inakabiliwa na changamoto kubwa katika siku zijazo.
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuratibu shughuli za maendeleo Bwana Khalid Malik anaona kuwa, tokea miaka ya 50 ya karne iliyopita, China imepita kipindi cha ongezeko la kasi la idadi ya watu, hata idadi ya watu bilioni 1.3 ya hivi sasa bado inaongezeka kwa milioni 10 kila mwaka. Serikali ya China imechukua masuala ya nguo, chakula, makazi na usafiri yanayohusika na familia kuwa masuala yanayopaswa kuzingatiwa kwanza.
Bwana Khalid Malik alisema kuwa, China ikiwa nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu duniani, imepata mafanikio makubwa ambayo hayakupatikana hapo kabla katika zaidi ya miaka 20 iliyopita, imewawezesha watu milioni mia kadhaa kuondokana na umaskini, na kukamilisha sehemu kubwa ya malengo ya maendeleo ya milenia ya Umoja wa Mataifa kabla ya wakati uliopangwa.
Waziri wa idadi ya watu na huduma za jamii wa Pakistan Bwana Husein alisema kuwa, Pakistan ni nchi ya 6 yenye idadi kubwa ya watu duniani, pia inakabiliwa na matatizo mengi sawasawa na yale yanayoikabili China. Serikali ya China inasifiwa na watu duniani kwa juhudi zake za kusukuma mbele maendeleo ya jamii na uchumi, kutokana na mafanikio hayo yaliyopatikana katika kusuma mbele maendeleo ya uwiano kati ya idadi ya watu na jamii nchini China. Nchi nyingi ikiwemo Pakistan zote zinataka kujifunza kutoka kwa China kwa kuipatia ushirikiano wa pande mbili mbili au pande nyingi.
Kutokana na Taarifa ya idadi ya watu na maendeleo ya nchi iliyotolewa na China, serikali ya China imetekeleza sera ya kimsingi ya nchi ya uzazi wa mpango kuanzia mwishoni miaka ya 70 ya karne ya 20, ikipunguza kwa kiasi kikubwa kiwango cha uzazi wa watu, ikadhibiti kwa ufanisi ongezeko la haraka la idadi ya watu, na pia imehimiza mabadiliko ya mtizamo kuhusu uzazi. Hivi sasa kiwango cha uzazi cha China kimepungua hadi kufikia kile cha nchi zilizoendelea duniani. Kutokana na kupunguza idadi ya watoto wanaotakiwa kutunzwa na kuongezaka kwa idadi ya watu wanaofikia umri wa miaka wa kufanya kazi, uchumi wa China unaongezeka kwa kasi.
Taarifa hiyo imedhihirisha kuwa, idadi ya watu na maendeleo ya China bado yanakabiliwa na masuala mengi mapya na changamoto mbalimbali ambazo zinatishia vibaya maendeleo na utulivu wa China wa siku za usoni. Kwa mfano, kiwango cha chini cha ongezeko la idadi ya watu kinadumishwa pamoja na ongezeko kubwa la idadi ya watu, ongezeko la haraka la idadi ya wazee, tofauti kubwa ya kijinsia kati ya watoto wachanga, ongezeko kubwa la watu wanaohamahama, shinikizo kubwa za kutafuta nafasi za ajira, na migongano inayoonekana dhahiri siku hadi siku kati ya idadi ya watu na uchumi, jamii, maliasili na mazingira.
Taarifa hiyo inaona kuwa, masuala hayo makubwa yakitaka kutatuliwa kwa wakati na kwa ufanisi, yanatakiwa kuzingatiwa kwa mawazo ya kuyapa kipaumbele maslahi ya watu, na kutimiza maendeleo endelevu ya uwiano katika nyanja zote, na kuzingatia upya na kurekebisha zaidi mikakati ya maendeleo ya idadi ya watu na mipango ya idadi ya watu.
Bwana Khalid Malik alipozungumzia suala kuhusu maendeleo endelevu ya familia pia aliainisha kuwa, ingawa China imepata maendeleo makubwa katika kusukuma mbele maendeleo endelevu ya uchumi, lakini maendeleo ya uchumi na mchakato wa utandawazi wa uchumi duniani umeleta changamoto nyingi kwa kutimiza maendeleo endelevu ya familia za China, China inatakiwa kushughulikia ipasavyo na kwa dharura masuala matano makubwa kuhusu kupunguza umaskini, kukamilisha mfumo wa huduma za jamii, uhamishaji wa idadi kubwa ya watu, tishio la ugonjwa wa ukimwi, na hali ya mazingira na viumbe inayozidi kuwa mbaya.
Idhaa ya Kiswahili 2004-12-09
|