Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-14 15:36:24    
Wanawake wapaswa kutoa mchango mkubwa zaidi katika maendeleo ya jamii nchini China

cri
Mkutano wa nne wa Kamati Kuu ya chama tawala cha China ulisisitiza kuwa maendeleo ya jamii hayawezi kutenganishwa na juhudi za wanawake, kwa hiyo namna ya kuhamasisha juhudi za wanawake katika ujenzi wa ustawi wa jamii ni kazi muhimu ya Umoja wa Wanawake, na pia ni fursa nzuri kwa wanawake wa China kuonesha uhodari wao wakiwa wanahitaji kuelewa vema na kusaidiwa na jamii nzima.

    Maendeleo ya jamii hayawezi kutenganishwa na ujenzi wa uchumi, kwa hiyo ni kazi muhimu kuwaongoza, kulinda haki zao, na kuwahamasisha washiriki kazi na ubunifu wa kazi. Mwaka huu miradi kama "Huduma Bora kwa Wakazi", na "Msaada kwa Watu Maskini", imetoa mchango mkubwa katika juhudi za kuleta nafasi za ajira, kuinua ujuzi wa kazi na kupanua wigo wa ajira. Habari kutoka mkutano wa 11 wa waendeshaji wa mashirika ya wanawake duniani zinasema kuwa, mashirika yanayoendeshwa na wanawake yaliyokumbwa na nakisi yanachukua asilimia 2 tu kati ya mashirika yote duniani, na ni wachache tu wanaojihusisha na ufisadi. Hii inamaanisha kuwa wanawake ni nguvu muhimu katika ukuaji wa uchumi.

    Usawa wa jinsia katika maendeleo ya jamii ni kitu cha lazima. Kutekeza kwa uthabiti sera ya msingi ya kuhakikisha usawa huo na kulinda maslahi ya wanawake ni muhimu sana. Mwaka huu viongozi wa mikoa 31 pamoja na miji mikubwa waliandika makala au kutoa hotuba kuhusu sera hiyo ya msingi ili kuinua ufahamu na umuhimu kuhusu usawa huo na hadhi ya wanawake nchini China. Hata hivyo, katika baadhi ya sehemu nchini China ukiukaji wa haki za wanawake unaendelea kutokea, kadhalika mambo ya biashara ya dawa za kulevya, ukahaba na biashara ya watoto wachanga, ajira za watoto wadogo na matumizi ya nguvu nyumbani yanaendelea. Hali kama hiyo kwa kiasi kikubwa imeathiri wanawake na watoto kiafya na kiroho na kuathiri utulivu wa jamii. Umoja wa Wanawake katika ngazi zote unapaswa kuwatetea wanawake wanaoathirika na kupambana na hali ya kukiuka haki zao. Na wanawake pia wanapaswa kupata elimu ya sheria ili kutumia elimu hiyo kama silaha ya kulinda maslahi yao.

    Maendeleo ya jamii hayawezi pia kutengana na malezi ya watoto, na kwenye suala hilo wanawake wanawajibika zaidi. Mwaka huu kamati kuu ya Chama imeagiza Umoja wa Wanawake kazi ya kusukuma mbele malezi ya nyumbani na imeanzisha harakati za "Kuwa wazazi wa kufaa na kuandaa watu hodari wanaofaa", na ilianzisha idara za aina nyingi za kutoa misaada ya elimu katika shule na familia na kwa familia zenye mazingira mazuri, maskini, familia za waseja na familia zenye wazazi wanaofanya kazi za kibarua mahali pengine.

    Maendeleo ya jamii hayawezi kutenganishwa na utulivu wa jamii, na familia ni shina la jamii, wanawake wanapaswa kutoa mchango katika kuleta furaha kwenye familia na kutunza maadili. Wanawake wanapaswa kuhusisha maslahi yao wenyewe na maslahi ya taifa. Wanawake ni nguvu kubwa katika kuleta utulivu wa jamii katika familia, katika sehemu za makazi ya mijini na viungani, na kuondoa migogoro ya aina mbalimbali na kuharakisha hatua za maendeleo ya jamii.

Idhaa ya kiswahili 2004-12-14