Kitoweo hiki cha kiislamu kinapendwa kwa kuwa kina viungo vichache na ni rahisi kukitayarisha
Mahitaji
Kilo 1.25 za nyama ya ng'ombe ya sehemu ya kati ya kidari, gramu 50 za mafuta ya karanga?kiasi kidogo cha sosi ya soya, chumvi, MSG, sukari, mvinyo wa kupikia, pilipili, vitunguu maji, tangawizi na vitunguu saumu vilivyosagwa, poda mweusi ya pilipili, aniseed
Njia
1. tia nyama ndani ya maji baridi pamoja na vitunguu maji, tangawizi na aniseed, pilipili na poda mweusi ya pilipili chemsha mpaka vichemke na nyama ikaribie kuiva.
2. kata nyama katika vipande bapa venye urefu wa kiasi cha sm 9, upana wa sm 3 na unene wa sm 1, vipange vizuri katika sahani.
3. tia mafuta ndani ya chungu na kuyapasha joto kwa moto wa kiasi. Mafuta yanapofika moshi, tia vitunguu, tagawizi na vitunguu saumu vilivyosagwa. Mara tu usikiapo vitu hivi vikinukia, tia sosi ya soya, mchuzi wa soya, supu, mvinyo wa kupikia, chumvi na sukari. Kisha tia vile vipande vya nyama kwenye chungu na uchemshe mpaka mchanganyiko wa vitu hivyo uchemke, punguza moto na endelea kupika kwa moto mdogo kwa dakika 6, ongeza moto tena, tia MSG. Kitoweo hiki sasa kiko tayari, kupakue katika sahani na andaa.
Nyama hii ya ng'ombe iliyoiva vizuri na yenye mchuzi mwekundu, huvutia na ina ladha nzuri.
|