Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-17 10:56:28    
Kitambaa cha Yunjin

cri

    China ni nchi iliyovumbua kufuga viwavi vya hariri na kufuma vitambaa vya hariri duniani. Katika zama za kale, "Jin" (kitambaa cha hariri kilichotiwa nakshi), kiliwakilisha kiwango cha juu, tulijua kufuma "jin" katika Enzi ya Shang. Ufumaji wa "jin" alistawi sana ilipofika Enzi ya Qing, wakati huo sehemu ya Kusini ya China ilikuwa kiini cha ufumaji wa hariri.

    Chimbuko la "Yunjin" ni mji wa Nanjin. Ina historia ya ufumaji ya miaka 700. Mji wa Nanjin uko kusini ya Mto wa Changjiang, una maji mengi, unafaa kwa kilimo cha miforosadi na kufuga viwavi vya hariri. Ufumaji wa kitambaa cha hariri uliendelea sana.

    Katika enzi ya Yuan, Ming na Qing, kitambaa cha "Yunjin" kiitumiwa kushona mavazi pamoja na kupamba mahekalu. Baadhi ya wakati, wafalme walikitumia kuwazawadia mawaziri wao. Katika vitu vilivyochimbuliwa kutoka makaburi 13 ya wafalme wa Enzi ya Ming vimegunduliwa vipande vya "Yunjin" vilivyozikwa pamoja na wafalme.

     "Yunjin" hufumwa kwa makini na kwa nyenzo safi. Wakati wa kufuma nyuzi nyingi za dhahabu zinatumika. Kuna aina tatu za "Yunjin" Nazo ni "Kujin", "kuduan", na "zhuanghua". Kati ya hizo "Zhuanghua" ni bora zaidi, na ilitumika kushonea mavazi ya wafalme katika zama za kale. Michoro iliyokuwepo kitambaa cha "Yunjin" huwa ni maua yanayomaanisha neema na baraka.

    Mwazoni mwa karne hii, kazi za mikono ziliachwa nyuma na kazi za viwanda vya kisasa. Ufumaji wa "Yunjin" ulififia siku hadi siku na ulikuwa karibu kutoweka kabisa kabla ya kuasisiwa kwa China Mpya. Oktoba 1956, hayati Waziri Mkuu Zhou Enlai aliagiza: "Kwa vyovyote vile nawaomba watu wa Nanjin wafufue ufumaji wa "Yunjin" na kuuendeleza." Desemba 1957 taasisi hiyo ilikusanya vitambaa vya "Yunjin", kuandika na kuhariri historia yake. Mafundi wazee waliwafundisha vijana ufumaji wa "Yunjin". Sasa si kama tu wameshajua kufuma "Yunjin" ya zamani, bali pia wamevunbua aina nyingine mpya za vitambaa vya "Yunjin".

Idhaa ya Kiswahili 2004-12-17