Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-22 19:15:21    
Sekta ya tiba na afya nchini China imepata maendeleo ya haraka katika miaka mitatu iliyopita tangu China ijiunge na WTO

cri
Mwanzoni wakati China kujiunga na WTO, baadhi ya watu walikuwa na wasiwasi kwamba, kutokana na kupunguzwa kwa ushuru wa forodha siku hadi siku, dawa za nchi za nje zitamiminika kwa kiasi kikubwa kwenye soko la China. Lakini je hali halisi ikoje ? mwandishi wetu wa habari alimhoji Naibu Mkurugenzi wa Kamati ya biashara ya tiba na dawa ya China Bw. Zhu Changhao, alisema kuwa, tangu China ijiunge na WTO, athari zilizotokea kwa makampuni ya dawa ya China siyo kubwa kama watu walivyokadiria, ambapo mwelekeo wa kuendelea kwa haraka. Anasema:

" sekta ya dawa za China imefunguliwa kwa nje mapema. Kabla ya kujiunga na WTO, makampuni mengi makubwa ya dawa ya nchi za nje yameanza kushirikiana na makampuni ya dawa ya China, makampuni hayo si kama tu yanatengeneza dawa nchini China, bali pia yanauza bidhaa zake nchini China."

Bw. Zhu Changhao alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, dawa zilizotengenezwa na makampuni ya ubia ya China na nchi za nje zinachukua 40% katika soko la China. Wakati huo huo, kiasi cha bidhaa za dawa zinazoingizwa kutoka nchi za nje kinapungua siku hadi siku.

Walipozungumzia athari nyingine kwa makampuni ya dawa ya China, Bw. Zhu Changhao anasema:

" kujiunga na WTO kumetuletea athari kubwa katika mawazo yetu ya kuendesha kampuni. Tumetuma watu wengi kujifunza uzoefu mzuri katika nchi za nje, na tumetumia uzoefu huo katika kazi. Hivi sasa kiwango cha utengenezaji wa dawa cha China kimeinuka juu zaidi kuliko zamani."hii inatusaidia kushiriki ushindani duniani.

Bw. Zhu Changhao alijulisha kuwa, kutokana na ahadi ilizotoa China wakati wa kujiunga na WTO, tarehe 11 mwezi Disemba mwaka huu, soko la biashara ya jumla na rejareja nchini China linapaswa kufunguliwa kwa nchi za nje kikamilifu. Lakinii aliona kuwa, kwa kuwa China imekuwa na makampuni makubwa kadhaa yanayofanya biashara ya rejareja ya dawa, hivyo makampuni za nchi za nje hayataleta athari kubwa mbaya katika soko la China.

Katika miaka mingi iliyopita, kwa kuwa China haikuwa mwanachama wa WTO, nchi nyingi ziliweka vikwazo kwa dawa ya kichina, maendeleo ya dawa za mitishamba za kichina yalizuiliwa katika soko la dunia. Lakini kutokana na kanuni za WTO, nchi wanachama za WTO haziruhisiwi kuwekeana vikwazo. Hivyo dawa za mitishamba za kichina ina nafasi nzuri kwa kuingia soko la dunia. Katika miaka mitatu iliyopita, idara husika za uendeshaji wa dawa ya kichina zilichukua hatua mbalimbali za kuimarisha ubora, usalama wa dawa mitishamba za China ili kuongeza nguvu ya ushindani kwa dawa ya kichina katika soko la dunia. Kuhusu hali hiyo, Mkuu wa idara ya ushirikiano wa kimataifa wa dawa za mitishamba za China Bw. Shen Zhixiang anajulisha:

" katika miaka ya hivi karibuni, China ilitumia fedha nyingi ili kuanzisha vituo viwili vya majaribio na utafiti wa dawa za mitishamba za China, ambapo vituo 7 vya uendeshaji wa shughuli za dawa za mitishamba za China vilianzishwa nchini China. Hivi sasa shughuli za utafiti na majaribio ya dawa za mitishamba za China zinatekelezwa kwa kufuata kiwango cha kimataifa."

Baada ya China kujiunga na WTO, wagonjwa wa kigeni wanaweza kutibiwa nchini China. Kutokana na ahadi ya China, wagonjwa wa kigeni wanapotibiwa nchini China wanaweza kupata huduma kama wachina walivyopata. Ikilinganishwa na nchi zilizoendelea, gharama za matibabu nchini China ni ndogo, hivyo wagonjwa wengi wa nje wanakuja nchini China kutibiwa. Naibu Mkuu wa Hospitali ya Huaxin ya Beijing Bw. Zhang Zongming alisema kuwa,

" muda si mrefu uliopita, mgonjwa mmoja wa moyo wa Canada alipata huduma katika hospitali yetu. Ingawa alitoka nchi iliyoendelea, lakini alitibiwa kama mchina alivyopata. Kwa mfano mgonjwa mmoja wa China akifanyiwa operesheni analipa Yuan mia 3, mgonjwa huyu wa Canada pia alilipa kiasi hicho."

Bw. Zhang Zongming alisema kuwa, tangu China ijiunge na WTO, kiwango cha huduma za tiba za China kinainuka siku hadi siku, wagonjwa wengi wageni wanakuja China kutibiwa. Hivi sasa, vyombo vingi vya matibabu vya hospitali hiyo vimeboreshwa ili kutoa huduma nzuri zaidi kwa wagonjwa wa nchi za nje.

Idhaa ya kiswahili 2004-12-22