Kutokana na hali ngumu inayoikabili China kuhusu kinga na tiba ya ugonjwa wa ukimwi, siku za hivi karibuni wizara ya afya ya China imependekeza kuanzisha harakati za kueneza ujuzi kuhusu kinga na tiba ya ugonjwa wa ukimwi, ili watu wa sekta mbalimbali za jamii waweze kuzingatia shughuli hiyo.
Katika mpango wa kueneza ujuzi kuhusu kinga na tiba ya ugonjwa wa ukimwi nchini kote, kituo cha uenezi wa ujuzi kuhusu ukimwi kitabuni alama, kufanya tathmini ya pande zote kuhusu hali ilivyo hivi sasa ya kazi hizo kuanzisha utarabibu wa kuhamasisha watu, kuweka masanduku ya vifaa husika vya uenezaji wa ujuzi, na kutekeleza kazi kwa sekta mbalimbali na watu mbalimbali. Harakati hizo ni pamoja na kukusanya, kuendeleza na kutoa matangazo ya radio na televisheni yanayohusiana na maslahi ya umma katika kinga na tiba ya ugonjwa wa ukimwi.
Katika "ripoti ya tathmini ya pamoja kuhusu kinga na tiba ya ugonjwa wa ukimwi" iliyotolewa tarehe 1 mwezi Decemba na wizara ya afya ya China na kikundi maalumu cha Umoja wa Mataifa kinachoshughulikia mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi nchini China, matatizo mengi yaliyopo katika kazi ya kueneza ujuzi kuhusu ugonjwa huo yalichambuliwa na kuelezwa, kama vile ukosefu wa mfumo mwafaka, kutokuwa na muda wa kutosha, na hali isiyo halali kuhusu ugawaji wa muda na sehemu ya uenezaji wa ujuzi. Ripoti hiyo inaonesha kuwa, uenezaji huo kwa kiasi kikubwa ulitekelezwa katika miji mikubwa, siyo tu haukutekelezwa mara kwa mara vijijini, bali pia haukuweza kuwa na athari kama inavyotarajiwa katika sehemu kubwa ya vijijini. Aidha maudhui na mifumo ya uenezaji huo ilikuwa ya aina moja tu ambayo hakukuwa na mambo mengi, haikulenga sekta mbalimbali wala watu mbalimbali, ilipuuza tofauti za sehemu, makabila na jinsia, haikuzingatia vya kutosha uenezaji ujuzi kuhusu kupambana na unyenyepa dhidi ya watu walioambukizwa virusi vya ugonjwa wa ukimwi, na kazi ya kueneza ujuzi kwa watu wanaohitaji kabisa kuelimishwa haikuwekwa kwenye ajenda za idara husika za serikali.
Mwaka huu, wizara ya afya ya China ililikabidhi shirika la uchunguzi la "Ling Dian" jukumu la kufanya uchunguzi na kutoa "ripoti ya ujuzi na maoni ya watu wa China kuhusu ugonjwa wa ukimwi mwaka 2004". Ripoti hiyo inaeleza kuwa, watu wa mijini na vijijini nchini China wanausikia mara kwa mara ugonjwa wa ukimwi lakini hawauelewi kwa kina ugonjwa huo kwa kina na kwa kawaida watu hao wana maoni ya unyenyepa na hofu kwa ugonjwa wa ukimwi na wagonjwa wa ukimwi. Hali hiyo imeifanya kwa kiasi fulani wizara ya afya na utibabu kutoa pendekezo hilo la mpango wa kueneza wa ujuzi kuhusu ugonjwa wa ukimwi.
Idhaa ya Kiswahili 2004-12-23
|