Kumiminika mijini kwa vibarua kutoka vijiji ni njia panda ya mchakato wa kuendeleza miji ya China na kuendeleza uchumi na jamii ya vijiji vya China, hivi sasa vibarua kutoka vijiji wamekuwa nguvu kazi muhimu katika shughuli mbalimbali, lakini kwa sababu ya mfumo wa China, hadhi yao na huduma zao lilikuwa ni tatizo.
Mwaka huu kadiri sera na sheria zilivyotekelezwa katika sehemu mbalimbali nchini China, hali hiyo imekuwa ikibadilika, na vibarua kutoka vijiji wamekuwa wenyeji wa mijini .
Mwezi machi mwaka huu idara ya ujenzi ya mkoa wa Gansu ilitangaza sera moja, ambayo inamtaka kila kibarua anayefanya kazi katika mradi wa ujenzi ulioanzishwa mwaka 2004 akatiwe bima ya ajali. Kibarua mmoja anayefanya kazi katika mji wa Lanzhou kutoka mji wa Baiyin, mkoani wa Gansu, aliposikia habari hiyo alisema kwa furaha kuwa yeye na wenzake wamefanya kazi mjini kwa miaka mingi, lakini walikuwa wanavijiji tu, kwa kuwa hawakuwa na vitu vyovyote mjini, lakini mwaka huu wanaweza kukata bima ya ajali, hali ambayo inawafanya wajisikie kama nao ni wenyeji wa mji huo.
Hii ni sera mojawapo kati ya sera nyingi zilizotolewa na serikali ya China mwaka huu, ambazo nia yake ni kulinda haki za vibarua. Katika sehemu mbalimbali nchini China, sera nyingi zimewapanga vibarua kwenye mfumo wa miji. Kwanza, serikali za sehemu kadhaa zimeanzisha mfumo wa kuweka dhamana ya fedha ili zitumike kuwalipa mishahara vibarua ambao hawajalipwa mishahara, na serikali za mitaa huwasaidia vibarua kupewa mishahara ili kutatua suala lililowasumbua vibarua la kutolipwa mishahara. Pili, mikoa mingi ikiwemo Hebei, Hunan, Zhejiang, Shangdong, Jiangsu, Sichuan imewapatia vibarua hadhi sawa na wakazi wa mijini, na katika mkoa wa Hebei, Anhui na mji wa Chongqing, vibarua wamepewa haki ya kukata bima ya matibabu, ambayo ilikuwa ni huduma kwa wakazi wa mijini katika siku za zamani, na hivi sasa katika mkoa wa Jiangsu, serikali imesamehe malipo maalum ya shule ya watoto wa wakulima wanaofanya vibarua mijini.
Katika mji wa Tianjin, Shanghai na Heilongjiang, mashirikisho ya wafanyakazi yamewashirikisha vibarua kutoka vijiji, hali ambayo imeainisha kuwa vibarua wamekuwa sehemu moja ya tabaka la wafanyakazi. Kujiunga na shirikisho la wafanyakazi kwa vibarua sio tu kutalinda haki halali za vibarua, bali pia kutasaidia vibarua kuingia katika maisha ya mjini.
Ili kutekeleza mpango uliobuniwa na wizara sita za China kuhusu kuwaandaa vibarua kutoka vijiji kati ya mwaka 2003 na 2010, sehemu mbalimbali zimezidi kuwaandaa vibarua, na inatarajiwa kuwa suala la kukosa ajira kutokana na hali ya kuwa na ujuzi hafifu litatatuliwa zaidi. Aidha, mwaka huu shughuli za burudani baada ya kazi za vibarua zinafuatiliwa na jamii nzima ya China.
Wataalam husika waliona kuwa ingawa sera hizo za hivi sasa hazijatekelezwa kote nchini China, lakini zinaonesha mwelekeo wa kuinua hadhi ya vibarua kutoka vijiji na kuwapatia huduma sawa na wakazi wa mijini katika duru jipya la mageuzi ya China.
Mwanasayasi wa jamii wa China, ambaye pia ni mtafiti wa taasisi ya sayansi ya jamii ya Gansu Bi. Bao Xiaoxia aliainisha kuwa?"Kama miji ikihitaji vibarua kutoka vijiji, inapaswa kuwapatia fursa ipasavyo. Vibarua kupata huduma sawa na wakazi wa mijini ni ni hatua kubwa inayoelekea lengo la kupunguza pengo kati ya miji na vijiji nchini China. China inapaswa kurekebisha uhusiano kati ya miji na vijiji na kufungua mlango wa miji kwa vijiji, huu ni msingi wa kutimiza lengo la kujenga jamii yenye maisha bora ya kimsingi kote nchini China."
Idhaa ya Kiswahili 2004-12-23
|