Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-24 16:21:54    
Liu Kunyan na michoro ya Ndani ya Chupa

cri

    Michoro ya ndani ni michoro iliyochorwa upande wa ndani wa kichupa cha kuwekea tumbaku ya unga. Liu Kunyuan mwenye umri wa miaka 41 ni mwanachama pekee na mkulima wa Jumuia ya Kimataifa ya Kichupa cha kuwekea tumbaku ya unga ya China. Michoro aliyochora ndani ya kichupa cha kuwekea tumbaku ya unga inajulikana sana katika sanaa hiyo.

    Mnamo Oktoba ya mwaka 1993, kwa mara nyingine alifika New York, Marekani kuhudhuria mkutano wa 25 wa Jumuia ya Kimataifa ya Chupa za Ugoro ya China, na alichora katika mkutano huo. Wajumbe 160 kutoka nchi 14 walisifu sana ufundi wake wa uchoraji.

    Bwana Liu ni mkazi wa kijijini. Mama yake ni fundi wa kukata karatasi na kutarizi. Kutokana na hali hiyo, tangu utotoni mwake, Liu alianza kuigiza michoro ya wachoraji maarufu. Alianza kuchora michoro ndani ya chupa za ugoro alipofikia umri wa miaka 25.

     Chupa za ugoro zenye michoro ya ndani ni sanaa ya kijadi ya China iliyoanza kutokea katika Enzi ya Qing. Wakati huo, maofisa walikuwa wanapenda kunusa ugoro; kwa hivyo, vilitokea vyombo vya kuwekea ugoro. Chupa za aina hiyo huwa ndogo na za kupendeza na husifiwa katika sekta ya sanaa ya duniani kuwa ni "sanaa ndogo iliyokusanya aina nyingi za sanaa za China".

    Wachoraji wa vipindi mablimbali walikuwa makini sana katika uchaguzi wa kalamu za kuchorea. Mwanzoni walitumia vipande vya mianzi, na baadaye brashi ilichukua nafasi ya mianzi. Bwana Liu hachoki kujifunza kwa unyenyekevu kutoka kwa walimu wake. Kutokana na msingi wa kutumia uchoraji wa kijadi pia amevumbua uchoraji mwingine. Anapendelea kuchora watu, milima, maua, miti, samaki, wadudu na pia huchora hadhithi za mapokezi. Michoro yake imewahi kununuliwa na kuthaminiwa na Wachina na watu wa nchi za nje.

Idhaa ya Kiswahili 2004-12-24