Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-24 20:38:40    
Ukimwi na ustaarabu wa maingiliano ya kijinsia

cri

     

Kwenye kongamano kuhusu "Ukimwi na Ustaarabu wa Maingiliano ya Kijinsia"lililofanyika hivi karibuni mjini Beijing wataalamu mashuhuri walitahadharisha kuwa maambukizi ya Ukimwi yameanza kuingia kwenye jamii ya watu wa kawaida kutoka jamii ya watu walio kwenye hatari zaidi ya kuambukizwa nchini China, na hatua ya kimsingi dhidi ya maambukizi ya Ukimwi ni kuimarisha kwa juhudi kubwa ustaarabu wa maingiliano ya kijinsia kote nchini China.

     Mwanasayansi wa taasisi ya elimu ya jamii katika Taasisi Kuu Sayansi ya Jamii ya China Bw. Li Yinghe, mkurugenzi wa Shirikisho la China la Kinga na Tiba ya Ukimwi Bw. Dai Zhicheng, na mkuu wa bodi ya wakurugenzi ya Jumuiya ya Jinsia ambaye pia ni profesa Xu Tianmin wa Chuo cha Matibabu katika Chuo Kikuu cha Beijing na profesa Zhang Konglai wa Chuo Kikuu cha Matibabu cha Beijing walijadiliana kwa kina habari na hali zilizotangazwa na vyombo vya habari, nazo ni kama "kukutana kimwili kati ya wanaume na wanawake itakuwa ni njia kuu ya kuambukiza Ukimwi nchini China", "mapambano dhidi ya tovuti za ukahaba yafanyika kwa mara ya kwanza nchini China", "kwa mara ya kwanza China yafanya uchunguzi kwa wanawake kuhusu tendo la kujamiana" na "mapendekezo ya idara sita kuhusu uenezi wa matumizi ya kondomu", na vipindi vya televisheni kwa mada ya tendo la kujamiana "barakoa". Kwa kauli moja wataalamu wanaona kuwa ingawa hivi sasa maambukizi kwa njia ya damu bado ni njia muhimu ya kuambukiza Ukimwi nchini China lakini uchunguzi unadhihirisha kuwa mwaka 2004 katika baadhi ya mikoa na miji, maingiliano ya kijinsia yamekuwa njia kuu ya kuambukiza Ukimwi, na ugonjwa huo umeanza kuenea miongoni mwa watu wa kawaida kutoka jamii ya watu walio katika hatari zaidi ya kuambukizwa. Ili kukabiliana na hali hiyo na kuleta matokeo mazuri katika juhudi za kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo ni lazima uimarishwe kwa kadiri iwezekanavyo ustaarabu wa maingiliano ya kijinsia kote nchini China.

   

Wataalamu wanaona kuwa katika ujenzi na uimarishaji ustaarabu wa kisasa wa maingiliano ya kijinsia lazima uachwe kabisa "mwiko wa kusema wazi kuhusu maingiliano ya kijinsia ila kutenda kisiri siri" na kubadilisha mwiko huo kuwa "kusema wazi na kutenda kiakili kwa pamoja". Wataalamu husika pamoja na jumuiya za sekta mbalimbali za jamii zapaswa kufanya utafiti kwa mapana na marefu kuhusu maingiliano ya kijinsia, kubadilishana maarifa na kuleta mfumo wa uenezi wa elimu ya maingiliano ya kijinsia ya kiafya, ya kiakili na kupata mawazo sashihi ya namna moja kuhusu maingiliano ya kijinsia katika jamii nzima. Kadhalika, elimu kuhusu maingiliano ya kijinsia pia ni lazima ienezwe miongoni mwa watu wazima na kupitia uenezi wa elimu hiyo ya kina na yenye matokeo mazuri kupunguza maambukizi ya Ukimwi, na kuwafanya watu wazima na hasa kundi la watu ambao ni rahisi kuambukizwa wawe na ufahamu. Zaidi ya hayo, ni haja kuenzi na kuheshimu maadili mema ya jadi ya China.

Idhaa ya kiswahili 2004-12-24