Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-24 20:50:05    
Mkuu wa ofisi ya mambo ya Afrika ya wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Cheng Tao azungumzia Afrika

cri

    Bw. Cheng Tao anayeshughulikia mambo ya kiafrika kwa miaka mingi anafahamu sana hali ya Bara la Afrika. Alipohojiwa na mwandishi wa habari kusimulia Afrika kwa maneno machache, alisema kuwa Afrika ni bara lenye historia ndefu, maeneo makubwa na maliasili nyingi, ingawa sasa bara hilo linakabiliwa na matatizo mengi, lakini lina mustakabali mzuri. Bw. Cheng Tao alieleza kuwa, Bara la Afrika lilikuwa sehemu ya chanzo cha kiasili cha binadamu, pia ni sehemu pekee ambapo visukuku vya aina mbalibali vya binadamu katika maendeleo ya sokwe kugeuza kuwa binadamu vimegunduliwa. Aliongeza kuwa, Bara la Afrika pia ina maliasili nyingi. Kati ya akiba ya jumla ya mapipa bilioni 8 ya mafuta yaliyogunduliwa mwaka 2001 duniani, mapipa bilioni 7 yako kwenye ghuba ya Guinea barani Afrika. Bw. Cheng Tao alisema kuwa, ingawa sasa nchi nyingi za Afrika zinakumbwa na maafa ya vita na umaskini, lakini iko siku zitayashinda kutokana maliasili kubwa, ardhi zenye rutuba na watu wakarimu kwenye bara hilo.

    Bw. Cheng Tao alisema kuwa, ingawa China iko mbali na Afrika, lakini watu wa China na Afrika wana uhusiano mzuri na urafiki mkubwa. Alieleza kuwa uhusiano huo unatokana na sababu nyingi. Kwanza, China ni nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani, wakati Afrika ni bara lenye nchi nyingi zaidi zinazoendelea. Pande zote mbili zinaafikiana katika kulinda mamlaka ya nchi, kutafuta maendeleo, kuendeleza uchumi na na kulinda amani ya dunia. Pili, China na nchi mbalimbali za kiafrika hazikuwa na uhasama katika historia, badala yake, zote zilionja maumivu ya kunyang'anywa na kunyanyaswa kutokana na utawala wa ukoloni. Uhusiano kati ya China na Afrika ni wa kirafiki na kindugu. Katika miaka mingi iliyopita, China na nchi za Afrika zinaelewana, kusaidiana na kuwasiliana kwa moyo wa kidhati, ambapo urafiki wa kijadi kati ya pande hizo mbili zinapatia mitihani ya muda na historia. Siku zote China imekuwa ikiunga mkono kithabiti mamlaka ya nchi za Afrika. Aidha, China imepeleka wataalam wa tiba, kilimo na kiufundi kwenye nchi mbalimbali barani Afrika. Ukilinganishwa na mabara mengine duniani, uhusiano kati ya China na Afrika una msingi kithabiti zaidi, wakati watu wa China na wa nchi za Afrika wana uhusiano wa kindugu, na kufanya ushirikiano wa kusaidiana.

    Bw. Cheng Tao alisema kuwa, kwa jumla, watu wa Afrika wanawachukua wachina kama ni marafiki wakubwa. Hata katika baadhi ya vijiji vilivyoko mbali ktuoka miji barani Afrika, wakazi wa huko wanapowaona wachina huwasalimia kwa lugha ya kichina "Ni Hao". Bw. Cheng alimwambia mwandishi wa habari kuwa, wakati watu wa Asia wanapokumbwa na matatizo, wanavijiji hawauliza kama wao ni wachina au la, wakiwa ni wachina huwasaidia kwa ukarimu.

    Bw. Cheng Tao alieleza kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, harakati za kitamaduni kati ya China na Afrika zinaendelea vizuri sana. Kwa mfano, mwanzoni mwa mwaka 1999, China iliandaa maonesho ya sanaa za kiafrika, ili kuwafanya watu wa China wapate fursa ya kufahamu Afrika. Vitu vya kisanaa vilivyooneshwa kwenye maonesho hayo viliwavutia wachina wengi na kusifiwa sana. Mwezi Oktoba mwaka 2000, Kongamano la Karne Mpya ya mawasiliano ya utamaduni wa China na Afrika lilifanyika hapa Beijing nchini China. Mwezi Agosti hadi Septemba mwaka huu, China pia iliandaa Safari ya Utamaduni wa China Barani Afrika katika nchi 11 za kiafrika, zikiwemo Afrika Kusini, Cameroons na Ghana. Harakati hiyo ni ya kwanza iliyoandaliwa na serikali ya China kwenye Bara la Afrika tangu kuasisiwa kwa China mpya. Kufanyika kwa harakati hiyo kumejulisha aina mbalimbali za utamaduni wa kichina kwa watu wa Afrika, na kupitia harakati hiyo, waafrika wamepata habari nyingi zaidi kuhusu hali ya China. Aidha, harakati hiyo inakuza ushirikiano wa kitamaduni kati ya China na Afrika.

    Bw. Cheng Tao alisema kuwa, licha ya mawasiliano ya utamaduni, katika miaka ya hivi karibuni, ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya pande hizo mbili vilevile unaendelea vizuri, wakati thamani ya biashara inaongezeka haraka mwaka hadi mwaka. Zamani watu wa Afrika wanajua vitu vidogo vinavyotengenezwa na China kama vile viatu, nguo na kufuli, lakini sasa bidhaa za hali ya juu za China kama vile televisheni, refrigerator pia zinawafurahisha waafrika. Bw. Cheng Tao alieleza kuwa, mbali na kukuzwa kwa kazi biashara, katika miaka ya hivi karibuni, wanaviwanda wengi wa China wanawekeza vitega uchumi, na kuanzisha shughuli zao barani Afrika. hali ambayo inasaidia nchi za Afrika kuendeleza uchumi na kuondoa umaskini.

Idhaa ya Kiswahili 2004-12-24