Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-27 15:32:05    
Mji wa Kunming wajenga sehemu na mitaa ya burudani za kiutamaduni ili kuwavutia watalii

cri
Mji wa Kunming una hali ya hewa nzuri, siku za majira manne ya huko ni kama siku za mchipuko. Mji huo wa utalii una historia ndefu tangu enzi na dahari, lakini katika miaka ya hivi karibuni, mji wa Kunming umekumbwa zaidi na jukumu la kuwapokea na kuwasindikiza watalii, hali hii haisaidii maendeleo ya shughuli za utalii za mji huo. Ili kubadilisha mwelekeo huo wa maendeleo, mji wa Kunming unajitahidi kujenga sehemu na mitaa ya burudani za kiutamaduni ili kuwavutia watalii kufika na kukaa huko kwa muda, sehemu na mitaa hiyo ya burudani itajengwa kwa kuzunguka Mto Panlong ambao ni mto mama wa mji wa Kunming.

Mabaki mengi ya kumbukumbu za historia na utamduni yaliyoko kwenye kando za Mto Panlong yataonekana tena kuwa ni mvuto kwa watalii. Hivi sasa "mtaa mmoja wa utalii na burudani wa Mto Panlong" unajengwa mjini Kunming, ili kuharakisha ujenzi na uendelezaji wa maliasili za utalii za Mto Panlong. Kuna maduka mengi zaidi katika sehemu uliko Uwanja wa Tiaoyuan na Uwanja wa Dongfeng katikati ya mji wa Kunming, na mfumo wa mawasiliano ya huko umeboreshwa zaidi, ambapo kuna miundo mbinu mizuri ya barabara, na miti mingi zaidi imepandwa huko, hata mapambo ya taa na mengineyo pia ni mazuri kuliko sehemu nyingine. Sehemu hiyo ikijengwa vizuri zaidi itawavutia zaidi watalii na kuwawezesha kukaa huko kwa muda. Ujenzi wa mtaa wa utalii na burudani unalenga kuonesha mandhari nzuri ya kimaumbile ya Mto Panlong, na vivutio vya kumbukumbu za utamaduni. Wakati wa kujenga mtaa huo, hifadhi ya mazingira itapewa kipaumbele ili kujenga vizuri mji wa Kunming kuwa mji wa bustani na soko la utalii, ili kupata ufanisi mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kiviumbe.

Maonesho ya kwanza ya shughuli za utamaduni ya Kunming yameonesha kuwa, "mtaa mmoja wa utalii na burudani wa Mto Panlong" utakuwa na urefu wa kilomita 6.8, ambapo yatajengwa madaraja yenye vivutio vya taa na maua ili kuwawezesha watalii kuangalia mandhari wakati wa usiku na kununua bidhaa za utalii.

Mtalii mmoja kutoka Guilin mkoani Guangxi alisema kuwa, mji wa Kunming una hali ya hewa nzuri sana na mwafaka zaidi kwa binadamu, yeyote anapofika huko anaweza kuvutiwa na mandhari yake na kutarajia mji huo utajengwa vizuri zaidi na shughuli zake za utalii zinawavutia watalii wengi zaidi.

Idhaa ya kiswahili 2004-12-27