Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-04 20:39:44    
China yasaidia wakulima kuongeza pato kwa kutumia mikopo ya nchi za nje

cri

    Kila siku alfajiri mkulima He Yanmei anamwamsha mumewe kwenda kufanya shughuli za uchukuzi kwa kutumia gari lenye magurudumu matatu la kilimo. Gari hilo lilinunuliwa na He Yanmei mwaka 2003 kwa thamani ya Yuan 2,000 za mkopo wa kusaidia watu maskini. Mkopo huo umewasaidia sana watu wa familia hiyo, kwani tangu waliponunua gari hilo, wakafanya shughuli za uchukuzi kusafirisha mizigo ya wanakijiji na kuwapeleka mahali wanapotaka kwenda, hivyo pato la ukoo huo liliongezeka kwa kiwango kikubwa.

    "Kutokana na gari hilo, pato la kila siku lilikuwa zaidi ya Yuan 50, hata lilifikia Yuan 100 au 200 katika baadhi ya nyakati, kiwango hicho ni cha juu kwa wakazi wa sehemu ya vijiji. Siyo sisi wenyewe tunaona mkopo huo unatusaidia, hata watu wengi wanasifu mkopo uliotolewa."

    Yuan elfu 2 ni fedha kidogo kwa wakazi wa mijini, lakini kwa wakulima wanaoishi katika sehemu maskini kama He Yanmei ni kianzio cha kuondokana na hali ya umaskini kwa ukoo wake. Kwa kuwa familia ya He Yanmei inaishi katika wilaya ya Nanzhao ambayo inatengana kwa umbali mkubwa na watu wengine, imekuwa nyuma kimaendeleo na kukosa habari kuhusu mambo ya kisasa na maendeleo ya sehemu nyingine. Lakini katika miaka ya karibuni, wakazi wengi wanashughulikia kazi za uchukuzi, kufuga samaki na kupanda miti ya biashara kwa kutumia mikopo midogo midogo iliyotolewa na serikali, hivi sasa maisha yao yanabadilika kila siku inayopita.

    Idara halisi iliyotoa mikopo kwa wakulima wa sehemu anayoishi He Yanmei ni chama cha ushirika cha kusaidia wakulima maskini wilayani Nanzhao. Kiongozi wa chama cha ushirika cha Nanzhao Gou Changyuan alisema,

    "Mikopo midogo midogo ilianza kutolewa mwaka 1995 kwa kujifunza uzoefu wa mbinu ya mambo ya fedha ya teknolojia ya trust wa sehemu ya vijiji nchini Bangladesh kwa kupitia taasisi ya sayansi ya jamii ya China, ambayo ilianzisha vituo vinne vya majaribio nchini China, wilaya ya Nanchong ni moja kati ya vituo hivyo vinne. Baada ya miaka 10, hivi sasa idadi ya koo za wakulima zilizopata mikopo yetu zimefikia 7,715, na thamani ya mikopo tuliyotoa imezidi Yuan milioni 65."

    Vituo hivyo vilivyoanzishwa na taasisi ya sayansi ya jamii ya China kikiwemo kituo cha wilaya ya Nanzhao, mitaji yake inatokana na mikopo yenye riba kidogo au misaada inayotolewa na mashirika ya kimataifa zikiwemo trust ya sehemu ya vijiji nchini Bangladesh na Benki ya Citi Group. Tokea katikati ya miaka ya 90 ya karne iliyopita, idara ya utafiti wa maendeleo ya vijiji ya taasisi ya sayansi ya jamii ya China imefikisha mitaji hiyo mikononi mwa wakulima kwa njia ya utoaji mikopo, kuwasaidia kujifunza teknolojia na kuendeleza uzalishaji mali ili kuongeza pato lao.

    Wakulima wa sehemu maskini wanapenda sana mikopo hiyo, ambayo inatolewa kwa mara moja na kurudisha fedha za mikopo kidogo kidogo, wakulima wengi wanarudisha fedha za mikopo bila matatizo. Nchini China hivi sasa kuna vyama vya ushirika zaidi ya mia moja vinavyotoa mikopo ya kuwasaidia wakulima maskini. Mikopo iliyotolewa na vyama hivyo imezidi Yuan bilioni moja. Wafanyakazi wa vyama hivyo vya utoaji mikopo midogo wanasimamia mitaji hiyo kwa uangalifu mkubwa na makini, wakijua kuwa misaada hiyo ilitokana na jumuiya ya kimataifa ya kusaidia wakulima maskini, na wanataka mitaji hiyo itumike kwa wakulima maskini na kuwa na ufanisi mkubwa zaidi.

    Wizara ya biashara ya China imeanzisha ofisi moja inayoshughulikia moja kwa moja usimamizi kuhusu miradi ya Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa ya utoaji mikopo midogo midogo. Mkurugenzi wa ofisi hiyo Bw. Bai Chengyu alieleza hali ya usimamizi huo wa mikopo hiyo,

    "Tumejenga mfumo wa usimamizi nchini, na tumeweka vigezo vya sekta yetu katika vyama vya utoaji wa mikopo midogo vilivyoko katika wilaya 48 nchini. Tuna utaratibu kamili wa uhasibu, mfumo wa habari, na kila mwaka tunafanya ukaguzi kwa vyama hivyo ili kuhakikisha kuwa mitaji inatumika kuendana na mikataba iliyosainiwa kati ya serikali ya China na mashirika ya kimataifa."

    Uendeshaji mzuri wa utoaji mikopo nchini China umepongezwa na wadhamini wa mashirika ya kimataifa zikiwemo Benki ya Dunia, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na Citi Group. Mashirika mengi yameimarisha nguvu ya uungaji mkono kwa wakulima maskini. Kwa mfano, Citi Group baada ya kutoa zawadi ya dola za kimarekani milioni 1 na laki 3 mwaka 2001, hivi karibuni ilitoa zawadi ya dola za kimarekani milioni 1 na laki 5, ambazo zitatumika katika kutoa mafunzo ya utoaji mikopo midogo midogo.

    Baadhi ya wataalamu wa masuala ya sehemu ya vijiji nchini China wamesema kuwa ingawa kuna mashirika mengine ambayo yanatoa mikopo midogo kwa wakulima, lakini kuna utaratibu mrefu kabla ya kupata mikopo yao, zaidi ya hayo mashirika hayo hayaweki wafanyakazi wengi katika huduma ya utoaji wa mikopo midogo midogo, na kuna hitilafu fulani katika sehemu za pembezoni na mipakani. Hivyo kuanzishwa kwa vyama hivyo vya ushirika vya utoaji mikopo midogo midogo nchini kutaziba pengo lililoachwa katika sehemu ya vijiji. Wataalamu wanatarajia kutakuwa na mashirika mengi zaidi ya kimataifa yanayofuatilia na kuunga mkono utoaji wa mikopo midogo kwa wakulima maskini nchini China.

Idhaa ya Kiswahili 2005-01-04