Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-06 15:40:06    
Wanafunzi wa vyuo vikuu vya China watafuta ajira kutokana na hali ilivyo

cri
Katika mwaka 2005 idadi ya wanafunzi watakaohitimu kutoka vyuo vikuu itafikia milioni 3, na idadi hiyo ni kubwa kabisa tokea China ianze kufanya mageuzi ya elimu mwaka 1999, hivyo hali ya wanafunzi watakaohitimu kupata ajira itakuwa ngumu kulingana na ya zamani. Habari kutoka wizara ya elimu ya China zinasema kuwa, mwaka 2005 idadi ya wanafunzi itaweka rikodi katika historia. Kutokana na hali hiyo, mawazo ya wanafunzi kujipatia ajira imebadilika.

    Zamani kigezo cha kwanza ya wanafunzi wa vyuo vikuu kuchagua ajira kilikuwa " mshahara na mustakbali wa kikazi". Lakini sasa wanafunzi wanazingatia zaidi ya hali ya siku za usoni katika mashirika waliyochagua. Uchunguzi unaonesha kuwa, hivi sasa matakwa ya wanafunzi wa vyuo vikuu yamepungua kiwango cha mshahara kuliko miaka miwili iliyopita. Kwa kawaida, mshahara wa kila mwezi kwa mwanafunzi aliyehitimu kutoka chuo kikuu ni Yuan 1500-3000, lakini 75% ya wanafunzi wanachagua mshahara wa chini ya Yuan 2000 kwa mwezi. Mbali na hayo, wanafunzi wengi wanapochagua ajira, hawalinganishi na masomo waliyosoma katika chuo kikuu, kama ajira hiyo ni nzuri wanafunzi wanaichagua tu. Hii inaonesha kuwa, wanafunzi wa vyuo vikuu hawajali kutotumia masomo yao. Kwa wanafunzi wale ambao hawakupenda kuacha masomo yao wakiwa chuoni, kuhitimu kutoka vyuo vikuu ni nafasi mpya ya kuchagua maisha.

    Kuhusu ukubwa wa makampuni, wanafunzi wana mawazo tofauti. Kwa mfano, katika chuo kikuu cha viwanda cha Hefei, mkoani Anhui, mwaka 2004 31% ya wanafunzi waliohitimu walichagua kufanya kazi kwenye makampuni yenye wafanyakazi chini ya mia 5, 19% walisaini mkataba na makampuni yenye wafanyakazi kati ya 500-1000, na 25% walichagua makampuni yenye wafanyakazi kati ya 1000-3000. fikra ya zamani yaani " kampuni kubwa ndio kampuni nzuri" imebadilika. Kwa kuwa makampuni madogo yana utaratimu wa uendeshaji wenye unyumbufu, na uwezo wa kila mmoja unaweza kutumika vya kutosha, hivyo makampuni madogo yanakaribishwa zaidi kwa wanafunzi siku hadi siku.

    Takwimu za uchunguzi zinaonesha kuwa, hivi sasa ajira zinazokaribishwa zaidi na wanafunzi waliohitimu kutoka vyuo vikuu ni kwamba, kampyuta, huduma ya habari, uchumi na mawasiliano. Makampuni hodari ya teknolojia ya mawasiliano kama LENOVO China, Shenzhou China, Datang China, IBM Marekani, Microsoft Marekani, HP Marekani yanakaribishwa zaidi na wanafunzi, na bila shaka ushindani kati ya wanafunzi waliotaka kupata ajira katika makampuni hayo ni mkali.

    Habari nyingine zinasema kuwa, tangu China ijiunge na WTO, ushirikiano na mawasiliano kati ya China na nchi nyingie yanaongezeka siku hadi siku, hivyo watu wenye uwezo wa lugha za kigeni wanahitajika sana, Hasa wanafunzi wao wanaosoma lugha ndogo, kwa mfano lugha za kiarabu, kikorea, kithailand, kitaliano, kihispania n.k wanatafutwa sana na makampuni ya biashara.

    Profesa wa chuo kikuu cha lugha za kigeni cha Shanghai Bw. Li Shaozhu alisema kuwa, kutokana na mahitaji ya jamii, chuo hicho kitaweka masomo mapya ya lugha za kigeni nayo ni lugha za Persia, na Indonesia.

Idhaa ya kiswahili 2005-01-05