Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-05 20:26:07    
Maendeleo mapya yapatikana katika ushirikiano wa kimataifa kati ya China na nchi nyingine duniani katika sekta ya safari ya anga ya juu

cri

    China ikiwa nchi kubwa inayofanya shughuli zinazohusika na safari za anga ya juu, katika mwaka 2004 ikishirikiana na nchi zilizoendelea na nchi zinazoendelea pamoja na jumuiya za kimataifa, zilianzisha shughuli nyingi za ushirikiano katika sekta hiyo na kupata maendeleo mengi mapya.

    Idara ya taifa ya safari za anga ya juu ya China ilifahamisha kuwa, kutokana na miradi iliyothibitishwa ya ushirikiano kati ya China na Russia katika sekta ya safari za anga ya juu, mwaka 2004 China na Russia zilisaini mikataba mingi. Kutokana na makubaliano ya ushirikiano kati ya China na Idara ya safari za anga ya juu ya Ulaya kuhusu utafiti wa sayari mbili kwenye nafasi ya anga ya juu ya dunia, idara hiyo ya Ulaya imetoa zana na uungaji mkono wa kiteknolojia na huduma kadhaa, hivi sasa mradi wa kutafiti sayari mbili kwenye nafasi ya anga ya juu ya dunia umekamilika. Huu ni mradi mkubwa wa kwanza wa ushirikiano kati ya idara ya safari za anga ya juu ya China na Idara ya safari za anga ya juu ya Ulaya, ambao umekuwa mwanzo mzuri wa ushirikiano kati ya China na Ulaya katika sekta hiyo.

    Serikali ya China na serikali ya Brazil pia zimesaini Makubaliano kuhusu ushirikiano wa teknolojia ya nafasi ya anga ya juu, China na Brazil zitaendelea kuanzisha ushirikiano kuhusu satellite za No.3 na 4 za utafiti wa maliasili za dunia. Mwaka 2004 China na Brazil zilisaini makubaliano ya kuthibitisha uzalishaji wa satellite, kufanya ushirikiano kwenye sekta ya teknolojia ya anga ya juu ili kusukuma mbele maendeleo ya uchumi na jamii ya China na Brazil. China na Ufaransa pia zimeanzisha utaratibu wa usawazishaji kuhusu ushirikiano kwenye sekta ya anga ya juu, pia China inajitahidi kufanya mawasiliano na Marekani.

    China imejitahidi kushiriki katika mambo ya Kamati ya anga ya juu ya Umoja wa Mataifa. Ili kutekeleza zaidi mapendekezo mbalimbali ya mkutano wa tatu wa anga ya juu

    Shughuli zilizoanzishwa na China na nchi husika kuhusu ushirikiano wa pande nyingi za Asia na Pasifiki kwenye sekta ya anga zinaendelea kwa juhudi, na maendeleo halisi yamepatikana katika kuanzisha jumuiya ya anga ya juu ya Asia ya Pasifiki. Tokea mwezi Februari mwaka 2004, serikali za China, Pakistan, Thailand na Peru ziliidhinisha kutia saini mkataba wa jumuiya ya Asia na Pasifiki ya ushirikiano wa anga ya juu, na serikali ya Argentina imekubaliwa kuwa nchi mchunguzi wa jumuiya hiyo. Nchi nyingine kama vile Bangladesh, Mongolia, Philippines, Malaysia, Korea ya kusini, Indonesia, Ukraine, na Brazil pia zinafanya utafiti kuhusu ushirikiano huo.

  

 

Idhaa ya Kiswahili 2005-01-05