Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-05 21:43:54    
Upigaji wa nyama ya ng'ombe pamoja na doufu ya kuokwa

cri

Mahitaji

Nyama ya ng'ombe--gramu 160,

doufu laini--vipande 4

vitunguu maji--vipande 3

kiasi kidogo cha tangawizi,

mafuta--vijiko 5,

mchuzi mwepesi wa soya--vijiko 2

mchuzi mzito wa soya-- 1/2 kijiko

sukari--2/3 kijiko,

wanga wa muhogo--vijiko 2,

maji--kikombe 1

unga wa nyama ya kuku-- kijiko 1 cha chai

chumvi --1/3 kijiko

kiasi kidogo cha mafuta ya sesame na pilipili manga

Njia

1.Osha nyama ya ng'ombe, na uikaushe. Kata nyama ya ng'ombe iwe vipande vyembamba, na kuviweka kwenye bakuli, tia mchuzi mwepesi wa soya 1/2 kijiko, sukari 1/3 kijiko, wanga wa muhogo kijiko 1 na mafuta vijiko 2, pamoja na nyama ya ng'ombe kwa muda wa dakika 20, halafu weka vipande vya nyama kwenye maji ya uvuguvugu na chemsha kidogo, toa halafu kausha.

2. kata doufu iwe vipande vipande na kutia kijiko 1 cha chumvi kwa muda wa dakika 30 na kuvitia ndani ya maji ya vuguvugu na kuchemsha kwa dakika 3 na uvipakue.

3. Tia mafuta yaliyokwisha chemshwa ndani ya sufuria, yapashe moto mpaka yawe na joto la nyuzi 50-60, tia tangawizi kidogo, mimina kiasi kidogo cha maji, mchuzi mwepesi wa soya, mafuta ya sesame, pilipili manga, sukari, chumvi na unga wa nyama ya kuku, halafu tia vipande vya doufu na uchemshe mpaka viungo hivyo vikaribie kukauka, tia nyama ya ng'ombe na endelea kuchemsha mpaka nyama iive, tia vitungu maji, halafu tia mchuzi mzito wa soya na wanga wa muhogo. Mpaka hapo kitoweo hiki kitakapo kuwa tayari, kipakue.