Katika hali ya kawaida, binadamu hutambua hisia za mwanzake ikiwemo ya hofu kwa kupitia macho yake. Katika toleo jipya la jarida moja nchini Marekani lijulikanalo kwa "The Nature" wanasayansi wa Marekani wamesema kuwa wamekuwa na wazo hilo jipya kuhusu mfumo wa ufahamu wa hisia za ubongo wa binadamu kutokana na mwanamke mmoja mwenye hitilafu katika ubongo wake, ambaye anashindwa kufahamu hisia ya hofu ya mtu mwingine katika hali ya kawaida.
Kabla ya hapo, madaktari waliona kuwa vidude viwili vilivyoko katika pande mbili za ubongo wa binadamu ni vitu muhimu vinavyotambua hisia ya hofu kwa binadamu. Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 38, alipata hitilafu katika vidude hivyo viwili ndani ya ubongo wake kutokana na kuugua, ni kweli kwamba kwake ni vigumu kutambua hisia ya hofu inayoonekana katika uso wa binadamu, lakini ana uwezo kamili wa kusikia hisia za furaha, hasira na huzuni.
Katika utafiti wao, wanasayansi wa chuo kikuu cha uhandisi cha California waliwaonesha watoto picha za nyuso za watu zenye hisia za aina mbalimbali, na kila mara kuwawezesha kuona sehemu fulani ya picha hizo, walitaka watoto kueleza hisia wa watu walio kwenye picha. Wanasayansi waligundua kuwa watoto walipoangalia picha hizo waliangalia zaidi sehemu za pua na pembezoni mwa midomo yao, ambazo ziliwawezesha kabisa kutambua hisia za furaha au hasira za watu walioko katika picha hizo. Lakini watoto walipooneshwa picha za nyuso zenye hisia za hofu, walikuwa waliendelea kuangalia midomo na pua zao, lakini waliruka sehemu ya macho yao, hivyo walisema kuwa watu wa kwenye picha walikuwa watulivu.
Wanasayansi walisema kuwa kutokana na majaribio yaliyofanywa, macho ni njia muhimu ya kugundua hisia ya hofu ya mtu, isipokuwa hisia za furaha na hasira zinaweza kugunduliwa kwa sehemu ya mdomo wa mtu. Katika jaribio lingile, wanasayansi waliwakumbusha mara kwa mara watoto waliokuwa wakiangalia picha waangalie macho ya mtu aliye kwenye picha, matokeo yake ni kuwa uwezo wao wa kutambua hisia ya hofu ulifikia kiwango cha mtu wa kawaida, isipokuwa uwezo wao huo ulidumu kwa muda mfupi, na ilibidi wakumbushwe mara kwa mara.
Wanasayansi walisema kuwa jaribio lililofanywa la kurejesha uwezo wa mwanamke huyo wa kutambua hisia ya hofu linathibitisha kuwa hitilafu ya vidude viwili vilivyoko katika pande mbili za ubongo inaweza tu kudhoofisha uwezo au njia ya kuchunguza wala siyo kama madaktari walivyoona hapo kabla kuwa inaweza kuharibu kabisa uwezo binadamu wa kutambua hisia za mtu zinazoonekana usoni. Wanasayansi wanaamini kuwa vidude hivyo vilivyoko katika ubongo vinafanya kazi za juu juu tu kuhusu kurekebisha njia za kuchunguza na kuangalia kwa ubongo, lakini vina mfumo pekee wa kutambua hisia ya hofu inayoonekana katika macho ya mtu.
Wanasayansi wanaona kuwa matokeo ya utafiti mpya si kama tu yanasaidia ufahamu wa binadamu kuhusu mfumo wa hisia wa binadamu, bali yana maana kubwa kwa tiba kuhusu tatizo la kuwa mpweke na magonjwa ya kutambua hisia za mtu mwingine.
Idhaa ya kiswahili 2005-01-12
|