1. Suti
Wanaume wanaofanya kazi kwenye makampuni makubwa wanapaswa kuwa na suti nzuri, na wanaponunua suti mambo muhimu wanayozingatia ni ubora na mtindo wa suti ni muhimu sana. Mbali na hayo, rangi za shati, tai na soksi zinapaswa kulingana na rangi ya suti.
2. mkanda
mkanda pia ni muhimu sana kwa nyaraka. Wanaume wanapovaa suti wanapaswa kufunga mkanda. Lakini jambo muhimu ni kuwa, mtindo na rangi ya mkanda inapaswa kuendana na ule wa viatu.
3. mkoba
watu husema kuwa, mfuko wa biashara unajaza mafanikio ya wanaume. ni vigumu kufikiri kuwa, meneja mmoja mwanaume anakwenda kwenye kampuni bila kuwa na mkoba. Kwa kawaida, mkoba huo unapaswa kukidhi mahitaji ya kazi ya kawaida. Kwa mfano kuweza kuhifadhi nyaraka, kadi za biashara, kalamu, simu ya mkononi na kompyuta ya mkononi. Rangi nyeusi na kahawa ni mwafaka.
4. saa ya mkononi
saa ya mkononi ni alama ya hadhi na tambua ya wanaume. Kuna aina tatu za saa za mkononi, nazo ni saa ya mitambo, saa ya quartz na saa ya elektroniki. Ni bora kuvaa saa ya mkononi ya mitambo, kwani inaweza kumsaidia mwanamme kuonesha uzuri wake.
5 kiberiti cha sigara
Kama wewe ni mvuta sigara, ambapo unafuata mwelekeo wa maisha ya kiwango cha juu na kiwango cha elimu, usitumie kiberiti cha kawaida kuwashia sigara. Hivyo kiberiti cha sigara chenye bei ya juu kitakidhi mahitaji yako vizuri.
6 miwani
Miwani yenye mitindo na ubora mzuri inamsaidia mwanaume kuonesha tabasamu yake. Kama watu wanavyosema, mwanaume anayevaa miwani anaonekana kuwa na elimu kubwa na uzoefu mkubwa wa maisha. Na mwanaume anayevaa miwani ya jua lazima ni mtu mwenye nguvu na kuwa na mwenye furaha maishani.
7 marashi
Wanaume wengi hawajali kutumia manukato, lakini kutokana na uchunguzi, wanawake wanapenda zaidi wanamume wanaotumia manukato. Lakini jambo muhimu ni kuwa, usitumie marashi au manukato mengi, wanaweza kukukimbia na kukukwepa.
Idhaa ya kiswahili 2005-01-12
|