Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-15 14:49:07    
Mito ya Masikio

cri

    Mito ya masikio imepata jina hilo kwa sababu sehemu yake ya katikati hubonyea ndani ili masikio ya mtu anayeutumia yasikandamizwe anapoulalia. Mito hiyo hushonwa kwa kitambaa cha pamba na kutiwa nakshi za tarizi huko Wilaya ya Qingyang, Jimbo la Gansu. Kuna aina nyingi za nakshi, na zinazoonekana kistadi. Kazi zote hufanywa kwa makini na akina mama wa vijijini. Sampuli za nakshi huazimana ama baina ya familia. Kwa kuwa wilayaya Qingyang haifikiki kwa urahisi, athari ya mambo ya kisasa ni vigumu kuingia, kwa hivyo sifa za asili za mito ya masikio zinadumu mpaka sasa.

    Eneo la Qingyang ni moja ya maneno ambayo Wachina wa awali waliishi na kuzaliana. Qingyang ilikuwa chimbuko la harakati za Mfalme Huangdi, ambaye alikuwa babu mzazi wa kizazi cha Kichina. Wenyeji wa eneo hilo walikuwa na mawazo makali ya uzawa na sifa pekee za utamaduni. Sanaa za kiwakilishi (totem), nazo pia zilistawi sana. Miongoni mwa vyombo vya towe vya zama za mawe vilivyochimbuliwa kutoka kwenye eneo hilo, nakshi za samaki na chura zilichukua sehemu kubwa, kwani wanyama hao huzaliana kwa wingi mno. Ndyio maana, wenyeji waliwatambikia. Vilevile, walidhani kuwa binadamu na maumbile ni kitu kimoja chenye maingiliano mema, katika ulimwengu binadamu na maumbile hutegemeana na kusaidiana. Maumbo ya mito ya masikio ya Qingyang yanafanana na yale ya samaki na chura, hii inamithilisha imani ya jadi ya wenyeji.