Vituo vya habari vya mtandao wa internet vikiwemo shirika la hifadhi ya wanyama la China, shirika la habari la China na tovuti ya umma vilishirikiana kufanya uchuguzi huo, uliofuatiliwa sana na wachina. Katika zaidi ya siku 20, watu wa sehemu mbalimbali za China, na wachina wanaoishi katika nchi za nje wapatao milioni tano walipiga kura.
Katibu mkuu wa shirika la hifadhi ya wanyama la China Bw. Chen Runsheng alisema kuwa, madhumuni ya shughuli hiyo ni kuimarisha mwamko wa watu katika kuhifadhi wanyama, na kuongeza ujuzi wa watu kuhusu wachina kuandaa michezo ya Olimpiki inayosaidia kuhifadhi mazingira na kuonesha utamaduni wa China. Kutokana na maoni ya watu waliopiga kura, hivi sasa watu wengi zaidi wanafuatilia siku za usoni za maisha ya binadamu na mazingira, na kuwa na wazo kuhusu maendeleo ya uwiano kati ya binadamu na mazingira ya kimaumbile.
Mwaka 2001 katika sherehe ya ufunguzi wa michezo ya wanafunzi wa vyuo vikuu duniani ujumbe wa nchi mbalimbali ulipoingia uwanjani ulitakiwa kunyanyua kibao cha jina nchi kilichoonesha ndege wa taifa, lakini wakati huo China ikikuwa haijathibitisha ndege wa taifa. Miaka 10 iliyopita, msichana mmoja Xu Xiujuan aliyekufa kutokana na kujaribu kumwokoa bata maji. Ajali hiyo iliwahuzunisha sana watu na kuonesha wachina wanapenda kuhifadhi wanyama pori. Mwaka 1960 mkutano wa hifadhi ya ndege duniani ulizitaka nchi mbalimbali duniani kuthibitisha " ndege wa taifa", hadi sasa zaidi ya nchi 50 zimethibitisha ndege wa taifa. Hivi sasa shughuli za kuhifadhi ndege ni alama ya kiwango cha hifadhi ya mazingira kwa kila nchi. Hivyo China inapaswa kumchagua ndege wa taifa.
Korongo mwenye kichwa chekundu (Red -crowned crane) ni ndege wa utamaduni wa jadi wa China, katika uchaguzi wa ndege wa taifa zaidi ya asilimia ya watu walimchagua Korongo mwenye kichwa chekundu (Red -crowned crane).
Hivi sasa mwamko wa wachina wa kuhifadhi mazingira umeimarishwa siku hadi siku. Zhalong ya mkoa wa Hei Longjiang ni maskani ya Korongo mwenye kichwa chekundu, msichana mmoja wa sehemu hiyo alieleza kuwa, serikali ilipeleka askari polisi kuhifadhi ndege hao. Mwaka 2003, sehemu hiyo ilikumbwa na hali ya ukosefu wa maji, mji wa Qiqi-haer ulipeleka maji kenda kwenye sehemu hiyo kwa miezi mitatu, mradi mwingine wa kupeleka maji pia unaendelea.
Daktari wa elimu ya baiolojia ya chuo kikuu cha walimu cha Hainan Bw. Liangwei alisema kuwa, kuchagua ndege wa taifa kunawasaidia watu kuongeza mwamko na wazo la kuhifadhi mazingira.
Idhaa ya kiswahili 2005-01-19
|