Wachambuzi wanaona kuwa, kwa kuwa ongezeko la uchumi wa nchi zilizoendelea kuwa la taratibu na serikali ya China kuchukua hatua za marekebisho na udhibiti wa uchumi, ongezeko la uchumi wa nchi zinazoendelea litapungua kwa kiasi fulani kwa mwaka 2005, lakini uchumi wa nchi zinazoendelea utaendelea kuwa na ongezeko kubwa.
Benki ya dunia imekadiria kuwa, ongezeko la uchumi wa nchi zinazoendelea litafikia asilimia 5.4 mwaka 2005, ingawa ongezeko hilo litakuwa chini ya kiwango cha mwaka 2004, lakini bado ni la juu kuliko lile la mwaka 2000 hadi mwaka 2003.
Kutokana na hali ya hivi sasa tunaweza kuona kuwa, hali ya uchumi wa sehemu muhimu zinazoendelea ni nzuri. Ongezeko la uchumi wa nchi zinazoendelea za Asia ya mashariki litaendelea kuchukua nafasi ya kwanza duniani, na mwelekeo wa maendeleo ya sehemu ya Asia ya kusini pia ni wa kasi sana. Sehemu ya Latin Amerika imejitoa kutoka janga la mgogoro wa fedha, na kushika njia ya ongezeko. Hali ya sehemu ya Afrika pia inaelekea kwa tulivu zaidi, na kuweka mazingira yanayosaidia maendeleo ya uchumi wa sehemu hiyo. Russia itaendelea kupata maslahi kutoka kwa hali ya kupanda juu kwa bei ya mafuta kwenye soko la kimataifa.
Benki ya dunia imekadiria kuwa, mwaka 2005, ongezeko la uchumi wa nchi za Asia ya mashariki litafikia asilimia 7 ambayo ni chini ya asilimia 7.9 ya mwaka 2004. Katika sehemu nyingine zinazoendelea, ongezeko la uchumi wa Asia ya kusini litafikia asilimia 6.3 kutoka asilimia 6, sehemu ya Latin Amerika na sehemu ya Caribbean kasi hiyo itapungua na kufikia asilimia 3.7 kutoka asilimia 4.7, sehemu za kusini mwa Sahara za Afrika itafikia asilimia 3.6 kutoka asilimia 3.2, sehemu za Ulaya na Asia ya kati kasi yake itapungua na kufikia asilimia 5.6 kutoka asilimia 7, na sehemu ya mashariki ya kati na sehemu ya Afrika ya kaskazini zitaendelea kuwa na ongezeko la uchumi la asilimia 4.7.
Mwaka 2005 utakuwa na sababu mbalimbali zinazoweza kusaidia nchi zinazoendelea kudumisha ongezeko la haraka la uchumi. Kwanza, kwa ujumla uchumi wa nchi zilizoendelea utadumisha ongezeko mwafaka, hasa uchumi wa Marekani unaelekea kuongezeka, hii itasaidia nchi zinazoendelea kuongeza uuzaji bidhaa nje. Shirika la ushirikiano na maendeleo ya uchumi limekadiria kuwa, ,ongezeko la uchumi wa nchi wanachama wake 30 litafikia asilimia 2.9 mwaka 2005, ingawa ni chini ya lile la asilimia 3.6 la mwaka 2004, lakini litakuwa la juu dhahiri kuliko lile la asilimia 2.2 la mwaka 2003.
Aidha, nchi kubwa zinazoendelea kama vile China na India zitaendelea na ongezeko la haraka la uchumi, ambalo litaendelea kusukuma mbele maendeleo ya uchumi wa kisehemu. Kamati ya Umoja wa Mataifa ya uchumi na jamii ya Asia na Pasifiki imekadiria kuwa, ongezeko la uchumi wa China litafikia asilimia 8.8 mwaka 2005, ambalo ni chini kidogo kuliko asilimia 9 ya mwaka 2004, na ongezeko la uchumi wa India litafikia asilimia 6.8 kutoka asilimia 6.
Zaidi ya hayo, baada ya kufanya marekebisho ya miundo ya uzalishaji kwa miaka kadhaa iliyopita, nguvu za uchumi wa nchi zinazoendela zimeongezeka kwa kiasi fulani, uwezo wao wa kupambana na changamoto na athari kutoka nje umeongezeka, na mazingira ya uwekezaji vitega uchumi yameboreshwa. Kwa mfano, mwaka 2004 bei ya mafuta ilipanda kwa kiasi kikubwa, lakini hali hii haikuleta athari mbaya sana kwa uchumi wa nchi zinazoendelea. Na upanuzi wa biashara ndani ya sehemu zinazoendelea pia ni nguvu kubwa ya kusukuma mbele ongezeko la uchumi.
Idhaa ya Kiswahili 2005-01-20
|