Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-21 15:12:41    
Serikali ya China yawafuatilia watu wenye matatizo ya kiuchumi

cri

Bwana Tian Jianhua na mke wake wanaoishi katika mtaa wa Chongwen mjini Beijing, na wote hawana kazi. Mtoto wao ni mwanafunzi, hivyo wana matatizo makubwa ya kiuchumi. Baada ya kupewa fedha za kumudu kiwango cha chini kabisa cha maisha, wameanza kuwa na tabasamu. Kama ilivyo kwa Bwana Tian Jianhua, wakazi wengine milioni 2.2 wa miji mikubwa na wastani wenye matatizo ya kiuchumi wanapewa fedha za aina hiyo.

Utaratibu wa China wa huduma za jamii za kumudu kiwango cha chini kabisa cha maisha unahakikisha maisha ya utulivu ya mamilioni ya wakazi wa mijini wenye matatizo ya kiuchumi kutokana na kupunguzwa kazini, kukosa ajira, ulemavu na kustaafu.

Kuwanufaisha raia kadiri iwezekanavyo ni agizo la kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China na baraza la serikali kwa kazi za idara zinazoshughulikia mambo ya raia katika ngazi mbalimbali. Takwimu zinaonesha kuwa, hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka jana, kigezo cha wastani cha fedha ya kumudu kiwango cha chini kabisa cha maisha kilikuwa ni yuan 159 kwa mwezi, serikali ya China ilitenga fedha yuan bilioni 10.2 kwa mwaka mzima. Kiasi hicho kiliongezeka kwa yuan bilioni moja kuliko mwaka uliotangulia. Miji, mikoa na mikoa inayojiendesha 12 nchini China imetunga sera mpya za utoaji huduma kwa watu wenye matatizo ya kiuchumi, watu milioni 3.28 wamepata faida kutokana na sera hizo, na fedha nyingine milioni 30 pia zimeshatengwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 440 za wazee nchini.

Ni kazi kubwa kwa nchi yenye idadi ya watu bilioni 1.3 kuanzisha mfumo wa kumsaidia kila mtu mwenye matatizo ya kiuchumi. Zaidi ya hayo, China inaendelea kusukuma mbele kazi ya kuwasaidia watu wenye matatizo ya kimaisha. Imefahamika kuwa, tokea mwaka jana, miji na mikoa 3 nchini China imeanzisha mfumo wa kutoa fedha za kumudu kiwango cha chini cha maisha vijijini, wilaya 1206 za China zimejiunga na mfumo huo ambao umewanufaisha watu zaidi ya milioni 4.5. Kwa wastani kila mtu anapewa yuan 600 kwa mwaka.

Zaidi ya hayo, mfumo wa kutoa msaada wa matibabu umeanzishwa mijini na vijijini. Ilipofika mwishoni mwa Novemba mwaka jana, miji na mikoa 26 nchini China ilikuwa imetunga miswada ya kutoa misaada ya matibabu vijijini, kuwafaidisha watu zaidi ya milioni 4.9, na vituo vya jaribio vya kutoa misaada ya matibabu mijini pia vimetoa huduma kwa wale wanaohitajika.

Ujenzi wa mfumo wa utoaji misaada mijini na vijijini pia ulianzishwa mwaka jana. Hivi sasa miji na mikoa 14 imeshaanzisha mfumo huo, mikoa mingine 12 inajiandaa kufanya mkutano wa kazi ya ujenzi wa mfumo huo.

Mwaka 2004, mageuzi na kuboresha mfumo wa kupambana na maafa ya dharura kuliwanufaisha mamia na maelfu ya raia wa kawaida. Tarehe 12 Agosti mwaka jana, kimbunga cha "Yunna" kiliukumba mji wa Wenling, mkoani Zhejiang. Baada ya saa moja tu, wizara ya mambo ya raia ya China ilizindua mpango wa kutoa msaada wa dharura, kazi ya usimamizi na utoaji tathmini kuhusu hasara zilizoletwa na maafa hayo zilifanyika baadaye.

Imefahamika kuwa, hivi sasa mfumo wa China wa kulimbikiza vifaa vya kupambana na maafa kimsingi umekamilika. China imejenga maghala 10 ya ngazi ya serikali ya kuhifadhi vifaa vya kupambana na maafa kama vile mahema, maji, chakula na zana za kupambana na baridi, vifaa hivyo vinaweza kuhakikisha mahitaji ya kimsingi kwa watu wanaokumbwa na maafa.

Idhaa ya kiswahili 2005-01-21