Habari kutoka idara ya afya ya mkoa wa Henan zinasema kuwa, mkoa huo utafanya upimaji wa virusi vya Ukimwi bila gharama kwa watu laki 6.3 mwaka huu.
Imefahamika kuwa, kutokana na kuelewa mweliko wa maambukizo ya Ukimwi mkoani Henan, idara ya afya ya mkoa wa Henan imetunga mpango wa upimaji wa Ukimwi katika mwaka 2005, miji 18 ya mkoa huo itatoa upimaji Ukimwi bila gharama kwa watu laki 6.3, wakiwa ni pamoja na watu wanaokabiliwa na hatari kubwa ya kuambukizwa, wajawazito na watu wanaojitolea damu bila malipo.
Hivi sasa, kuna watu elfu 25 walioambukizwa Ukimwi mkoani Henan, na serikali katika ngazi mbalimbali nchini China na sekta mbalimbali za jumuyia zinawafuatilia sana, idara ya matibabu pia inatoa matibabu mwafaka.
|