Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-24 16:01:53    
Twende Mlima Wudang kutafuta waumini wa dini ya kidao wanaofanya mazoezi ya Gongfu (zaidi)

cri

Dini ya kidao ni dini ya kienyeji nchini China, ambayo imekuwa na historia zaidi ya miaka 1800. Watu wanaoshughulikia kwenye mahekalu ya dini ya kidao wanaitwa Daoshi, ambao kila siku baada ya kufanya mazoezi ya dini ya kidao pia wanapenda kufanya mazoezi ya Gongfu. Katika sehemu ya kaskazini magharibi ya mkoa wa Hubei, katikati ya China, kuna Mlima Wudang ambapo ni sehemu maarufu takatifu ya dini ya kidao. Kwa zaidi ya miaka mia kadhaa iliyopita, Mlima Wudang unajulikana nchini na ng'ambo kwa vilele vyake virefu vya kupendeza na dini ya kidao yenye nguvu inayong'ara.

Tukizungumzia Mlima Wudang, tunapaswa kumzungumzia mfalme Yongle wa Enzi ya Ming ya miaka 600 iliyopita, ambaye ni mfalme maarufu katika historia ya China. Ili kuonesha heshima ya madaraka ya mfalme, mfalme huyo alituma wajenzi zaidi ya laki 3 na kutumia miaka 10 kujenga majengo zaidi ya 30 ya dini ya kidao. Majengo hayo yote yalikuwa majengo ya kifalme ya Enzi ya Ming kama yalivyo majengo ya Kasri la kifalme la Beijing. Hivyo majengo hayo ya Mlima Wudang pia yamesifiwa kuwa ni "Kasri la kifalme kwenye miamba". Mwaka 1994, majengo hayo ya Mlima Wudang yaliorodheshwa na Shirika la UNESCO la Umoja wa Mataifa kuwa urithi wa mali za utamaduni duniani.

Tukifunga safari kutoka Wuhan, mji mkuu wa mkoa wa Hubei, baada ya saa 7 tutafikika kwenye Mlima Wudang, halafu tutapanda basi kuingia kwenye sehemu yenye mandhari nzuri ya Mlima Wudang. Tukifuata njia inayozunguka na kupanda mlima, tunaweza kuona mashamba ya chai, miti mbalimbali adimu, na nyumba ndogondogo zilizojengwa vizuri. Kwenye sehemu ya Mlima Wudang, kuna vilele vikubwa na vidogo 72 vya mlima, na majengo ya mahekalu yaliyojengwa kwa mitindo mbalimbali yako ndani ya vilele vya mlima. Kilele cha Tianzhu ni kilele kirefu kabisa kwenye Mlima Wudang, na ndani ya kilele hicho kuna Ukumbi wa dhahabu ambao ni jengo maarufu kabisa kwenye Mlima Wudang, hivyo kilele hicho pia kinaitwa kuwa ni Kilele cha dhahabu.

Tukifika kwenye kilele cha dhahabu kwa kufuata njia nyembamba inayopanda mlima, tukipita milango kadhaa ya Ukumbi wa dhahabu na kupita majengo kadhaa madogo ya kale, tutafika kwenye Ukumbi wa dhahabu. Ukumbi huo ulijengwa kwenye jiwe la msingi, urefu wake ni zaidi ya mita 5. Ingawa ni karibu miaka 600 imepita tangu ukumbi huo ujengwe, lakini rangi yake ya dhahabu bado inang'ara. Lakini ukumbi huo haukujengwa kwa dhahabu halisi, bali ni kwa shaba na dhahabu. Inasemekana kuwa ukumbi huo ulijengwa kwa tani 20 za shaba na kilo 300 za dhahabu, ukumbi huo ni ukumbi mkubwa kabisa wa shaba wa China. Tukikaribia kwenye ukumbi wa dhahabu, tunaweza kuona waumini wa dini ya kidao wakiabudu mbele ya miungu na kuomba kwa malaika.

    

Kwenye Ukumbi wa dhahabu, inaabudiwa sanamu ya Mfalme mkuu Zhenwu mwenye nywele zilizotawanya mabegani na miguu ikiwa peku, sura yake ni sawa na ile ya mfalme Yongle wa Enzi ya Ming. Bwana Guo Zaizhu ambaye amefanya kazi kwa zaidi ya miaka 20 kwenye sehemu ya Mlima Wudang alituambia kuwa, sanamu za Mfalme mkuu Zhenweu zinazoabudiwa kwenye Mlima Wudang zote zilifinyangwa kwa kufuata sura ya Mfalme Yongle wa Enzi ya Ming aliyependa kutawanya nywele zake mabegani na kuwa miguu peku.

Wiki ijayo tutaendelea kuwasimulia hadithi kuhusu Ukumbi wa dhahabu na sanamu ya Mfalme mkuu Zhenwu kwenye Mlima Wudang.

Idhaa ya kiswahili 2005-01-24