Kabla ya miaka mitatu iliyopita serikali ya China ilitenga fedha nyingi kujenga mradi wa mabomba ya kupeleka ges ya sehemu ya magharibi kwa sehemu ya mashariki ya China. Mradi huo wa mabomba yenye urefu wa kiasi cha kilomita 4,000 unakusudia kupunguza hali ya upungufu wa nishati ya sehemu ya mashariki ya China. Katika zaidi ya mwaka mmoja uliopita mradi huo ulianza kupeleka ges kwa sehemu ya mashariki hatua kwa hatua, na ilipofika mwishoni mwa mwaka jana, mradi huo ulianza rasmi shughuli zake za kibiashara. Ebu katika kipindi hiki cha leo nitakueleza kazi muhimu unazorfanya mradi huo wa ges.
Sehemu za mashariki na kati ni sehemu zenye nguvu na ongezeko kubwa la kiuchumi nchini China. Sehemu hizo zinahitaji nishati nyingi lakini zina upungufu mkubwa wa nishati. Sehemu ya magharibi ya China, ambayo ina rasilimali nyingi za ges ya asili lakini maendeleo ya uchumi yako nyuma sana yakilinganishwa na sehemu nyingine nchini. Ili kutatua suala la upungufu wa nishati la sehemu za mashariki na kati na kusaidia sehemu ya magharibi kupata masoko kwa maliasili zake, China ilianzisha ujenzi wa mradi wa kupeleka ges ya sehemu ya magharibi kwa sehemu ya mashariki mwaka 2002. mradi huo unaogharimu fedha ya Yuan za Renminbi bilioni 140 ni mradi wa kwanza wa kusafirisha nishati nchini China kwa ukubwa, urefu wa mabomba, na kugharimu fedha nyingi.
Mko wa Henan, ambayo uko katika sehemu ya kati nchini China ni moja ya mkoa uliofaidika mapema kutokana na mradi huo. Mwezi Okatoba mwaka 2003 viwanda na wakazi wa mji wa Zhengzhlu, mji mkuu wa mkoa huo walianza kutumia ges ya asili iliyopelekwa huko na mradi huo. Mwandishi wetu wa habari alipotembelea huko hifi karibuni alimhoji mwanamke mmoja bibi Chang Yan aikisema kuwa ingawa sehemu yao ilianza kutumia ges ya asili zaidi ya miaka kumi iliyopita, lakini gei ilikuwa haitoshi kulingana na mahitaji ya wakazi, lakini hali lya hivi sasa ni tofauti kabisa tangu walipoanza kutumia ges ya asili iliyopelekwa huko na mradi huo. Alisema,
"Kabla ya Zhengzhou kupata ges ya asili ya sehemu ya magharibi, wakati watu wanapopika chakula baada ya kurejea nyumbani kutoka kazini, kwa kuwa watu wengi wanatumia ges kwa wakati mmoja, ges ilikuwa kidogo sana, na ilihitaji muda mwingi sana kwa kupika chakula, lakini hivi sasa ges ni nyingi sana."
Shanghai ni mji mkubwa kabisa wa viwanda na shughuli za biashara nchini China, hivi sasa mji huo ni soko kubwa kabisa la mradi huo wa ges ya sehemu ya magharibi. Kutokana na mpango uliowekwa, ges ya asili inayopelekwa huko Shanghai ni kama theluthi moja ya jumla ya ges ya asili inayopelekwa na mradi huo wa ges. Mwanzoni mwa mwaka 2004, mradi huo ulianza kupeleka rasmi ges ya magharibi kwa mji wa Shanghai. Naibu meya wa Shanghai Bw. Zhou Yupeng alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa ingawa maendeleo ya uchumi ya Shanghai ni ya kasi sana, lakini Shanghai ni "sehemu maskini" kwa rasilimali, 85% ya ges ya asili inayohitaji Shanghai itakiwa kupelekwa huko kutoka sehemu nyingine kila mwaka. Ofisa huyo alisema kuwa ges inayopelekwa huko na mradi wa ges ya magharibi imekuwa dhama kwa maisha ya wakazi wa Shanghai, ges ya asili inayotoka sehemu ya magharibi ya China itafanya kazi muhimu sana kwa maendeleo ya uchumi ya Shanghai. Alisema,
"Mwaka 2003 Shanghai ilitumia jumla ya ges ya asili karibu mita za ujazo bilioni 1, lakini katika mwka 2004 matumizi ya ges ya asili yaliongezeka kwa mara dufu, na ongezeko hilo lilikuwa ni ges iliyopelekwa hapa kutoka sehemu ya magharibi. Wakazi wa Shaghai hawana wasiwasi tena kuhusu ges ya asili tangu ges hiyo kuleta hapa kutoka sehemu ya magharibi, na wanaipenda sana kwa kuzilinganisha makaa ya mawe na nishati za aina ningine."
Naibu meya huyo alisema kuwa kwa kuvutiwa na mradi wa kupeleka ges, hivi sasa idadi ya familia zinazotumia ges ya magharibi imeongezeka hadi kuwa milioni 1 na laki 3 kutoka familia laki kadhaa ya hapo awali.
Mradi wa kupelaka ges ya sehemu ya magharibi kwa sehemu ya mashariki licha ya kubadilisha ya hali ya upungufu wa nishati iliyokuweko toka muda mrefu uliopita, bali pia umeleta manufaa kwa sehemu ya magharibi ukiwemo mkoa wa Xinjiang. Kwa mfano, zaidi ya Yuan bilioni 20 ya fedha zilizowekezwa katika mradi huo wa ges ya asili, ziliwekezwa mkoani Xinjiang kwa uendelezaji wa ujenzi wa visima vya ses ya asili. Mbali na hayo vifaa vya ujenzi, mitambo na nyingi ya zana zilizohitajiwa vilinunuliwa huko Xinjiang, hali ambayo imechangia maendeleo ya uchumi wa Xinjiang, mkurugenzi Liu Yanliang wa kamati ya maendeleo na mageuzi ya mkoa unaojiendesha wa Xinjiang alisema kuwa mradi wa kupelaka ges ya sehemu ya magharibi kwa sehemu ya mashariki umehimiza maendeleo ya uchumi wa mkoa wa Xinjiang kwa kutumia hali bora ya maliasili ya huko. Alisema,
"Mradi wa kupelaka ges ya sehemu ya magharibi kwa sehemu ya mashariki umepiga hatua ya kwanza madhubuti katika kubadiliha hali bora ya rasilimali kuwa hali bora ya maendeleo ya mkoa wa Xinjiang. Makaa ya mawe ya Xinjiang yanachukua 40% ya jumla ya makaa ya mawe nchini China, ges ya asili inachukua 34%, katika siku za baadaye mwelekeo wa maendeleo ya uchumi ya Xinjiang ni kubadilisha hali bora ya rasilimali kuwa hali bora ya uzalishaji na maendeleo ya uchumi."
Idara husika imefanya makadirio kuwa baada ya mradi wa upelekaji wa ges ya asili kufanya kazi, gesi ya asili ambayo imegunduliwa kwa hivi sasa ni zaidi ya mita za ujazobilioni 600, itaweza kupelekwa kwa miaka 30.
Idhaa ya Kiswahili 2005-01-25
|