Roboti moja lilisogea bila wasiwasi kwenye kitu kilichomethilisha cha kulipuka, lilikichukua, kugeuka nyuma na kukitupa katika mtungi wa kukinga mlipuko uliokuwa karibu nalo. Ndani ya dakika chache tu, tukio moja la hatari sana likaepushwa. Hiyo ni hali aliyoshuhudia mwandishi wetu wa habari, ambayo ni jaribio lililofanywa katika maabara ya chuo kikuu cha mawasiliano cha Shanghai. Habari zinasema kuwa roboti la aina mpya lijulikanalo kwa "Super-D" lililosanifiwa na kutengenezwa kwa kusudi la kukabiliana na mabomu yaliyotegwa na magaidi, limeorodheshwa katika orodha ya miradi inayosaidiwa na serikali na kujulikana kwa mpango wa "863" wa China.
Mtafiti wa idara ya maroboti ya chuo kikuu cha mawasiliano cha Shanghai profesa Yang Ruqing pamoja na watafiti wengine wakitumia muda wa zaidi ya miaka minne walifanikiwa kutengeneza roboti hilo lenye urefu wa sentimita 170, upana wa sentimita 70, kimo cha sentimita 120 na uzito wa kilo 200. Roboti hilo linaweza kutembea kwa kasi ya mita 40 kwa dakika, linaweza kupanda mtelemko wenye digri 40.
Mtaalamu huyu wa kupambana na milipuko lina umbo la kama gari moja lenye magurudumu 6, magurudumu manne yaliyoko chini yanatumiwa kwenda mbele na kugeuka, magurudumu mengine mawili yaliyoko mbele kwa juu yanatumika kwa kupanda mtelemko. Mkono wa roboti uko katika sehemu ya mbele. Ingawa roboti hilo lina mkono mmoja tu, lakini uwezo wake ni mkubwa na unaweza kufanya kazi za aina nyingi. Kwa kuendeshwa na mhandisi, mkono wake huo unaweza kurefushwa na kufupishwa zaidi, kukujwa na kuzunguka.
Profesa Yang Ruqing alieleza kuwa mtaalamu huyo wa kupambana na milipuko ana macho matatu ili aweze kuona vizuri zaidi. Jicho lake la kwanza ni lenzi ya kamera ya video, ambalo limewekwa kwenye upande wa mbele wa mkono. Jicho la pili ni lenzi ya kuchunguza na jicho la tatu, ambalo limewekwa chini yake na kutumika wakati wa kwenda mbele.
Idhaa ya kiswahili 2005-01-25
|