Mwezi Januari mwaka huu, kikundi cha wafanyabiashara wa Hongkong kilifanya uchunguzi wa kiuchumi kwa siku tano katika mkoa wa Hei Longjiang, Kaskazini-Mashariki mwa China ili kuwekeza vitega uchumi mkoani humo.
Bibi Chen Lei ni meneja mkuu wa kampuni ya biashara ya Qimao ya Hongkong, alipozungumzia uchunguzi mkoani Hei Longjiang alisema kuwa, kabla ya kufika hapa, aliona kuwa, uchumi wa sehemu ya kaskazini-mashariki ya China si mzuri, lakini alipofika Hei Longjiang nilishangaa sana, miji ya sehemu hiyo ni mikubwa, na uchumi uliendelea vizuri sana. Hivyo, aliona kuwa watu waliofanya kazi na kuishi katika Hongkong wanapaswa kuielewa zaidi uelewa wao China bara hasa sehemu ya kaskazini-mashariki ya China.
Kikundi hiki cha wafanyabiashara cha Hongkong kiliundwa na watu 26, kutokana na mwaliko wa kamati kuu ya mkoa wa Hei Longjiang na shirika la muungano wa vijana la mkoa wa Hei-Longjiang, kikundi hicho kilifanya ziara ya biashara ya siku 5 mkoani humo tangu tarehe 19. wafanyabiashara hao wengi ni watu wenye umri kati ya miaka 20 na 30, walitoka kwenye makampunimbalimbali ya Hongkong yakiwemo sayansi na tekolojia ya hali ya juu, uwekezaji vitega uchumi, vyakula, sheria, ustawi wa jamii.
Wafanyabiashara wa Hongkong walitembelea miji ya Harbin, Daqing, Daxing-anling, wakifanya ukaguzi wa uchumi na biashara, kufanya mazungumzo, ambapo mafanikio makubwa yalipatikana katika matembezi yao. Kwa mfano kampuni ya peremende ya Meisi ya Hongkongilitenga mtaji wa yuan milioni 10 huko mji wa Yichun ili kuanzisha kampuni moja ya kutengeneza asali; kampuni ya Dongli ya Hongkong ilitoa yuan milioni 50 ili kuanzisha kiwanda cha kutengeneza vifaa vya kujenga mwili.
Mbali na hayo, wafanyabiashara walipeleka sampuli nyingi za bidhaa za maji ya madini, mvinyo wa matunda, njugu mawe, mbegu za misonobari na uyoga, walipanga kuanzisha njia yao kusambaza bidhaa hizo kwenye sehemu za Hongkong, Makao na sehemu ya Mashariki ya Kati.
Ofisa wa shirika la serikali ya China lililoko Hongkong Bw. Pan Yonghua alisema kuwa, mwanzoni wafanyabiashara kadhaa vijana wa Hongkong walikuwa na wasiwasi kuhusu safari yao mkoa wa Hei-longjiang. Kwa kuwa hali ya hewa ya kaskazini-mashariki ni baridi mzizimo , na sehemu mbili ni mbali sana, licha ya walikuwa wanafikiri kuwa, uchumi wa sehemu ya kaskazini-mashariki ni duni na bado ni uchumi wa mipango. Lakini baada ya uchunguzi mawazo yao yalibadilika na waliona kwamba, mkoa wa Hei-longjiang ni sehemu ya kuvutia, yenye mazingira mazuri ya uwekezaji, walitaka kuimarisha zaidi maingiliano kati ya wafanyabiashara wa China bara na Hongkong.
Idhaa ya kiswahili 2005-01-26
|