Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-01 16:07:07    
"Mfalme wa vinywaji" nchini China

cri

Bw. Zong Qinghou mwenye umri wa miaka 60 mwaka huu, anaonekana ni pande la mtu, ingawa anapoongea sauti yake siyo kubwa, lakini maneno anayosema yanafahamika wazi kabisa. Kabla ya miaka 18 iliyopita katika mkoa wa Zhejiang, sehemu ya mashariki ya China yeye akishiirikiana na watu wdngine wawili walikopa Yuan kiasi cha laki moja, walianzisha kiwanda kidogo cha chakula, na kuanza kufuata njia ya biashara kutoka kuuza chakula cha barafu kilichouzwa kwa bei ya senti nne. Tokea hapo kiwanda chake kilimarika hatua kwa hatua hadi kuwa kiwanda kikubwa kinachozalisha vinywaji na chakula. Miaka minne baada ya kujenga kiwanda kidogocha chakula, walianzisha kampuni ya Wahaha mjini Hangzhou, ambapo walianza kufanya biashara kubwa ya chakula.

Kampuni ya Wahaha baada ya kuendelezwa kwa miaka mitano, hivi sasa imekuwa moja ya kampuni kubwa maarufu inayozalisha chakula hapa nchini. Hata hivyo, Bw. Zong Qinghou hakuridhika na hali ya hivi sasa, ameanza kufikiri namna ya kufanya kampuni yake kupiga hatua kbuwa zaidi katika maendeleo yake. Hivyo ameamua kufanya ubia na kampuni ya kimataifa.

Wakati alipovutia mitaji ya nchi za kigeni, Bw. Zong Qinghou anashikilia kuwa na nafasi kubwa zaidi za kuongoza usimamizi wa kampuni na kutaka kampuni ya kigeni inayoingia ubia isiwaachishe kazi wafanyakazi wa zamani wenye umri wa miaka zaidi ya 45. Wakati alipohojiwa na mwandishi wa habari Bw. Zong Qinghou alieleza sababu ya kufanya hivyo.

Alisema, "tunapovutia mitaji ya kigeni, lengo letu hasa ni kutumia mitaji na teknolojia yake kutusaidia kupiga hatua kubwa zaidi za maendeleo, hivyo tunapoanzisha kampuni ya ubia, tunataka kuwa na uamuzi katika kuendesha uzalishaji mali, la sivyo tunaonekana kama tunatoa kiwanda chetu kwa watu wengine. Kwa upande mwingine, kampuni yetu iliimarika kwa kutegemea wafanyakazi hao wa zamani, hivyo si vizuri utaratibu wa ubia kuathiri maslahi ya wafanyakazi wa zamani."

Hivi sasa kampuni ya Wahaha ya Hangzhou imekuwa ya kwanza kwa ukubwa hapa nchini na kuwa ni moja ya kampuni kubwa za vinuywaji duniani. Kampuni hiyo ambayo imekuwa na wafanyakazi karibu elfu 20, hivi sasa inazalisha maji baridi ya chupa, vinywaji vya soda na matunda pamoja na dawa za kuimarisha afya, na pato la kampuni limezidi Yuan bilioni 6. Takwimu moja inaonesha kuwa miongoni mwa kila chupa 6.25 zinazouzwa nchini, moja ilizalishwa na kampuni ya Wahaha.

Kampuni ya Wahaha inayo9ongozwa na Bw. Zong Qinghou imevumbua maajabu mengi katika sekta ya uzalishaji wa vinywaji, moja linalofurahisha watu zaidi ni kuzalisha cola ya China ijulikanayo kwa "Feichang Kele", ambayo maana yake ni furaha isiyo ya kawaida. Katika hali ambayo Coca-Cola na Pepsi karibu zimejazana kila mahali nchini China, kuingia kwenye soko ambalo limedhibitiwa na wafanyabiashara wa sekta ya vinywaji lilikuwa kama ni jambo la mwiko.

Kama wote wajuavyo kwamba Coca-Cola na Pepsi zimechukua nafasi kubwa sana katika sekta ya vinywaji duniani. Kampuni hizo mbili za kimataifa ziliingia kwenye soko la Chinatokea mwishoni mwa miaka ya 70 ya katne iliyopita, nakuchukua zaidi ya nusu ya nafasi katika soko la vinywaji nchini China. Baada ya kufanya uchnguzi Bw. Zong Qinghou aligundua kuwa ingawa kampuni hizi mbili za kimataifa zimeingia nchini

China miaka mingi iliyopita, lakini bado hazijajiendeleza katika sehemu ya vijiji vya China. Baada ya kuona nafasi kubwa ya biashara, kampuni ya Wahaha ilianza kuzalisha Feichang Kela miaka minane iliyopita na kutoa changamoto kwa Coca-Cola na Pepsi. Watu wanaifananisha mbinu ya biashara ya Bw. Zong Qinghou kuwa ni sera za kuizingira miji kutoka sehemu kubwa ya vijiji, lakini Bw. Zong Qinghou hakubaliani na msemo huo. Alisema, "Tunachofanya sisi ni kukwepa nguvu yake na kwenda kwenye sehemu ambazo kampuni hizo mbili hazina nguvu. Tulitangulia kuingia katika masoko hayo ya sehemu ya vijiji au miji iliyokuwa nyuma kimaendeleo. Hivi sasa Coca-Cola na Pepsi hazina nia ya kwenda katika sehemu hizo, na sisi tumekuwa na hali bora katika sehemu hizo."

Bw. Zong Qinghou alisema kuwa wakati walipoingia kwenye masoko hayo ya sehemu ya vijiji, walijitahidi kupunguza gharama ya uzalishaji ili kuwawezesha wakulima wapate Feichang Kele kwa bei rahisi zaidi. Zaidi ya hayo kampuni ya Wahaha iliwawekea nafasi kubwa wafanyabiashara wanaouza kinywaji cha Feichang Kele, hatua ambayo imefanya kinywaji cha Feichang Kela kuwekwa katika nafasi ya mbele katika maduka ya wafanyabiashara. Hivi sasa mauzo ya Feichang Kela yanazidi tani laki 6 kwa mwaka, na yanachukua nafasi kubwa mwaka hadi mwaka katika soko la vinywaji vya soda nchini China. Ingawa hivi sasa Coca-Cola na Pepsi bado zinachukua nafasi kubwa katika miji na sehemu zilizoendelea nchini China, lakini masoko ya sehemu kubwa ya vijiji vya China karibu yote yamekaliwa na kinywaji cha Feichang Kela cha kampuni ya Wahaha .

Baada ya kufanikiwa katika mauzo ya Feichang Kela, Bw. Zong Qinghou anatupia macho soko la Marekani ambayo ni sehemu asilia ya kuzalisha Coca-Cola. Mwezi Aprili mwaka 2004, kampuni ya Wahaha ilipeleka chupa laki 9 za Feichang Kele katika masoko ya Marekani na kupata mafanikio. Bw. Zong Qinghou amedokeza kuwa hivi sasa kuna kampuni nyingi za Marekani zinaomba kuuza kinywaji cha kampuni ya Wahaha.

Katika mahojiano, mwandishi wetu wa habari aligundua hali moja inayotatanisha kwamba Kampuni ya Wahaha inayoongoza katika sekta ya vinywaji hapa nchini, haina bodi ya wakurugenzi, Bw. Zong Qinghou yeye ni mkurugenzi mkuu na meneja mkuu wa kampuni, tena katika kampuni hiyo hakuna naibu meneja mkuu, hivyo anayeamua mambo yote ya kampuni hiyo ni wa Bw. Zong Qinghou peke yake, hata uamuzi wa kiwanda cha uzalishaji kilichoko chini ya kampuni hiyo wa kununua gari la kusafirisha bidhaa unapaswa kufanywa na Bw. Zong Qinghou yeye mwenyewe. Wakati mwandishi wetu wa habari alipoumwuliza kama usimamizi wa kazi wa namna hiyo utaathiri maendeleo ya kampuni, Bw. Zong Qinghou alisema, "Ninakiri kuwa usimamizi wa namna hiyo ni kama kujitwalia madaraka yote ya kampuni, lakini naona njia hiyo ni sahihi, hivi sasa tukitaka kufanikisha kampuni, tunapaswa kuwa na uongozi imara, ambao ni kama wa udikteta."

Mwishoni Bw. Zong Qinghou alisema kuwa mwaka 2005 kampuni ya Wahaha itazalisha bidhaa za aina mpya za chakula na vinywaji, tena itaingia katika sekta mpya za kazi za viwanda za kemikali za kijeshi na za matumizi ya watu wa kawaida na kuendeleza kampuni hiyo kuwa ya kimataifa.

   

Idhaa ya kiswahili 2005-02-01