Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-08 19:37:01    
Kukuza uwezo wa uzalishaji wa kilimo ni jukumu la kimkakati

cri
    Waraka wa "Maoni ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China na baraza la serikali kuhusu sera za kukuza uwezo wa uzalishaji wa kilimo" unasema kuwa, hivi sasa na kipindi cha siku za baadaye tunatakiwa kuuchukulia ukuzaji wa uwezo wa kuimarisha ujenzi wa miundo mbinu ya kilimo, kuharakisha maendeleo ya sayansi na teknolojia ya kilimo na uzalishaji wa mazao ya kilimo kuwa ni jukumu muhimu na la haraka.

    Mwaka 2004, kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China na baraza la serikali vilibuni sera nyingi za kuhifadhi na kuhimiza juhudi za wakulima na kuleta hali nzuri. Lakini tunapaswa kuona kuwa hivi sasa kuna mambo mengi yanayokwamisha maendeleo ya uchumi wa vijiji, yakiwemo miundo mbinu duni ya kilimo na uwezo mdogo wa uzalishaji wa kilimo. Ujenzi wa miundo mbinu ya kilimo ya China bado ni dhaifu sana, hususan katika upande wa ujenzi wa miradi ya maji mashambani na uwezo mdogo wa kukabiliana na maafa ya kimaumbile. Hivi sasa ni asilimia 39 ya mashamba ya mazao ya kilimo yanaweza kumwagiliwa maji, na theluthi mbili ya mashamba yanazalisha mazao chini ya kiwango cha wastani. Ni asilimia 40 tu ya mafanikio ya utafiti wa kisayansi na kiteknolojia ambayo yanatumika katika uzalishaji wa mazao ya kilimo, ikilinganishwa na kiasi cha 70% ya mafanikio ya kisayansi na kiteknolojia yanayotumika katika mambo ya kilimo katika nchi zilizoendelea. Udhaifu wa mfumo wa uenezaji wa teknolojia ya kisayansi katika ngazi za mashina unatokana na upungufu wa wahandisi wa kilimo. Muundo usio wa mwafaka wa uzalishaji mazao ya kilimo, sekta chache tu zinazohusika na uzalishaji wa mazao ya kilimo, nyongeza ya thamani inayotokana na mazao ya kilimo ni ndogo na viwanda vinavyohusika na usindikaji wa mazao ya kilimo huwa ni vidogo. Pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watu na ujenzi wa miji, mashamba ya kilimo yanapungua mwaka hadi mwaka. Upungufu mkubwa wa maji na matatizo mengine pia yanachangia kukwamisha maendeleo ya kilimo. Serikali kuu ya China inachukua ukuzaji wa uwezo wa uzalishaji mazao ya kilimo kuwa mkazo unaotiwa katika kazi za sehemu ya vijiji za mwaka huu, hatua hiyo ni yenye muhimu. Kukuza uwezo wa uzalishaji mazao ya kilimo ni muhimu sana katika suala la usalama wa chakula. China ina idadi ya watu bilioni 1.3, suala la chakula ni muhimu kabisa, kama China ikitaka kulisha idadi kubwa ya watu kwa mashamba machache yaliyopo na kutiwamizia watu mahitaji yanayoongezeka kwa mfululizo, basi inapaswa kujenga msingi imara wa kuwa na ongezeko katika uzalishaji wa nafaka; wakati huo huo kuna haja ya kuongeza kwa mfululizo pato la wakulima, kutumia ipasavyo uwezo wa uzalishaji wa kilimo, ambao bado haujatumiwa, kuongeza ufanisi wa uzalishaji wa kilimo na kuongeza kiasi cha uzalishaji wa nafaka katika kila hekta ya mashamba. Kwa upande mwingine China inapaswa kuendeleza ujenzi wa viwanda na miji, kuendeleza mambo ya kisasa ya kilimo na kuinua kiwango cha mambo ya kisasa ya kilimo.

    Kukuza uwezo wa uzalishaji wa kilimo ni kuhimiza uzalishaji wa nafaka na ongezeko la pato la wakulima, na kufanya utatuzi wa migongano ya hivi sasa uende sambamba na maendeleo ya muda mrefu. Kuzingatia uwezo wa kukabiliana na maafa ya kimaumbile pamoja na uwezo wa kukabiliana na migogoro ya kimasoko; kuinua kiwango cha uzalishaji wa mazao ya kilimo ya mashamba, pamoja na kuimarisha nguvu ya ushindani ya mazao ya kilimo; ni njia nzuri ya kuondoa upungufu wa rasilimali, na pia ni sera za kimsingi za kuimarisha nguvu ya maendeleo ya kilimo. Kama masuala hayo yakishughulikiwa ipasavyo, kutakuwa na msingi imara wa maendeleo endelevu ya kilimo.

    Kukuza uwezo wa uzalishaji wa kilimo ni kukuza uwezo wa pande nne wa msingi wa kuimarisha na kuboresha sera za kuunga mkono kilimo, ambazo ni kama ifuatavyo:

    Upande wa kwanza ni kukuza uwezo wa uzalishaji wa mazao na matumizi ya rasilimali ya ardhi. Kutekeleza utaratibu wa usimamizi makini kabisa wa ardhi, kuhifadhi vizuri ardhi, hususan mashamba ya kimsingi, kuhakikisha kwamba kiasi cha mashamba, matumizi pamoja na ubora wa mashamba havibadiliki. Kujitahidi kuongeza ubora wa mashamba, kuharakisha uboreshaji wa mashamba yanayozalisha mazao chini ya kiwango cha wastani, kuharakisha urutubishaji wa mashamba, kuwahamasisha wakulima wathamini, kuhifadhi na kuboresha mashamba. Pia kuna haja ya kujitahidi kuimarisha ujenzi wa miradi ya maji mashambani, kuimarisha ujenzi na kuboresha mashamba yanayomwagiliwa maji, kuhimiza mageuzi ya mfumo wa usimamizi pamoja na utaratibu wa umilikaji mali wa miradi midogo ya maji ya sehemu ya vijiji, na kueneza kwa haraka teknolojia ya kupunguza matumizi ya maji yanayotumika kumwagilia mashamba pamoja na kuzalisha mazao yanayohimili ukame.

    Wa pili ni kukuza uwezo na matumizi ya uvumbuzi wa sayansi na teknolojia ya kilimo. Tunatakiwa kuimarisha nguvu ya kuunga mkono utafiti wa kisayansi wa kilimo na kuharakisha mfumo mpya wa utafiti wa sayansi na teknolojia ya kilimo.

    Wa tatu ni kukuza uwezo wa mitambo na huduma za kilimo. Tunatakiwa kuharakisha matumizi ya mitambo katika kazi za kilimo, kuboresha mfumo wa huduma ya mitambo ya kilimo, kuzalisha pembejeo bora na imara, za bei nafuu na salama. Kuendelea kuhimiza uunganishaji wa uzalishaji wa mazao ya kilimo na usindikaji wa mazao ya chakula. Kurekebisha muundo wa matumizi ya fedha ya kilimo na kuimarisha ujenzi wa maeneo saba ya kilimo yakiwemo uzalishaji wa mbegu na mifugo bora.

    Wa nne ni kukuza uwezo wa wakulima wa kujiendeleza. Wakulima ni nguvu kuu ya uzalishaji wa kilimo. China ina nguvukazi milioni mamia kadhaa katika sehemu ya vijiji, ambao ni rasilimali kubwa ya maendeleo ya kilimo na uchumi wa taifa. Tunatakiwa kuimarisha elimu ya lazima katika sehemu ya vijiji ili kuongeza sifa na uwezo wa kazi ya wakulima.

    Tukiendelea na juhudi hizo kwa miaka kadhaa, uwezo wa kilimo wa China hakika utakuzwa zaidi na kuwa nguvu kubwa kwa maendeleo endelevu ya kilimo na kuwa na maongezeko ya uzalishaji wa mazao ya kilimo na mapato ya wakulima.

Idhaa ya Kiswahili 2005-02-08