Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-08 19:38:43    
Tepe nyekundu, alama ya kimataifa ya kinga na tiba ya Ukimwi

cri
    Tepe nyekundu ni alama ya kimataifa ya kina na tiba ya Ukimwi, alama hiyo ilianza kutumika mwishoni mwa miaka ya 80 ya karne iliyopita.

    Kwenye mkutano wa kwanza wa Ukimwi duniani watu wenye virusi vya Ukimwi walitoa wito wa kuwataka watu wawatambue, tepe nyekundu iliyo ndefu ilitupwa juu ndani ya ukumbo wa mkutano, waliounga wito huo waliipokea wakaikata kuwa vipande vipande na wakatia kifuani kwa pini.

    Baadaye, jumuiya nyingi na idara nyingi za afya duniani zilijipatia jina kwa "Tepe Nyakundu". Siku hadi siku alama ya tepe nyekundu imekuwa alama ya kimataifa ikimaanisha kuitaka dunia nzima izingatie tatizo la kinga na tiba ya Ukimwi, iwatambue na kuwajali watu wenye virusi vya Ukimwi.

    Tepe nyekundu imekuwa kama kiungo cha kuunganisha pamoja watu wa dunia nzima katika mapambano dhidi ya Ukimwi na kuwashughulikia wagonjwa hao, ikimaanisha jinsi binadamu wanavyothamani uhai na kutamani kuishi kwa amani, na pia ikimaanisha watu wanavyoshiriki katika mapambano hayo kwa "moyo wa dhati".

    Wenye virusi wa Ukimwi mkoani Yunnan China wapata tiba bure

    Juhudi za kuwatibu watu wenye virusi vya Ukimwi kwa tiba ya Kichina zitafanyika mwaka huu mkoani Yunnan China, kiasi cha watu hao 1000 watahudumiwa bure kwa tiba ya Kichina.

    Mkoa Yunnan ni moja ya mikoa iliyotiwa mkazo katika kinga na tiba Ukimwi nchini China. Kutokana na uchunguzi, tiba na dawa za Kichina za ugonjwa huo zina sifa za kuwaongezea wagonjwa uwezo wa kinga, kuboresha, kutuliza na kudhibiti hali ya ugonjwa, na zina sifa za kuinua hali njema ya kuishi, hazina madhara kwa afya na bei nafuu. Kwa kuikabili hali mbaya ya maambukizi ya Ukimwi, mkoa huo utaanzisha kazi ya tiba ya Kichina kwa majaribio katika mji wa Kunming na sehemu zinazojiendesha za makabila madogo madogo ya Wajingpo, Wabai, Wahani, na Wali mkoani humo.

    Idara ya afya ya mkoa wa Yunnan inataka idara zote za afya mkoani zishiriki na kutafiti tiba ya Kichina ya ugonjwa huo, na zianzishe pia matibabu ya Kichina na ya Kizungu kwa mchanganyiko, na katika sehemu zenye watu wengi wenye virusi HIV vianzishwe vikundi vya wataalamu kwa ajili ya maulizo ya tiba ya Kichina na kuandaa wahudumu wa tiba ya Kichina na pia tiba ya Kizungu ya Ukimwi.