Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-11 21:10:31    
Kikundi cha kwanza cha uchukuzi cha ulinzi wa amani cha China nchini Liberia

cri
    Tarehe 9, Desemba,mwaka 2003, kikundi cha kwanza cha usafirishaji cha ulinzi wa amani cha China kiliondoka kutoka Uwanja wa Ndege wa Beijing na kwenda nchini Liberia. Tarehe 5 Januari mwaka 2005, kikundi hicho kilirudi China baada ya kumaliza kazi yake kwa mafanikio. Katika mwaka uliopita, walisafirisha watu elfu 70 na vitu vya huduma tani elfu 30. Walionesha sura nzuri ya jeshi la China kwa nidhamu ya makini, moyo wa dhati na ufundi wa juu, Kamanda wa Jeshi la ulinzi wa amani la Umoja wa Mataifa nchini Liberia alikisifu kikosi hicho ni "No.1" kati ya vikundi mbalimbali vya ulinzi wa amani.

    Ili kuhakikisha kazi ya ulinzi wa amani inatekelezwa vizuri, kikundi cha uchukuzi cha ulinzi wa amani cha China kilifanya maafadalizi mazuri sana kabla ya kwenda Liberia. Naibu mkuu wa kikundi hicho Bw. Wang Qiusheng alieleza kuwa, umri wa wastani wa askari wa kikundi hicho ni miaka ya 27. Askari hao wanapaswa kuwa na uzoefu wa kuendesha magari kwa miaka 5, na kupitia uchunguzi makini sana wa uwezo wa mwili na sifa nzuri yakisaikolojia. Bw. Wang alieleza kuwa, kikundi hicho kilifanya mazoezi kwa makini sana kwa kufuatana na Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa mazoezi na mitihani ya kazi ya uchukuzi, pia kiliwaalika wataalamu wa saikolojia kutoa mafunzo, ili kuinua uwezo wa askari hao kukabiliana na hali hatari.

    Bw. Wang Qiusheng alipokumbuka safari hiyo nchini Liberia alieleza kuwa, kikundi cha uchukuzi cha China ni cha kipekee kati ya majeshi ya Umoja wa Mataifa nchini Liberia. Kazi ya kikundi hicho ni kusafirisha askari wa ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia, vitu vya huduma vinavyohitajika katika vituo mbalimbali vya kijeshi kama vile mafuta, maji na vifaa vya ujenzi, pamoja na vifaa vya Ujumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwenye sehemu mbalimbali nchini humo na katika uwanja wa ndege na bandarini. Katika mwaka uliopita, kikundi hicho kilifanya uchukuzi katika vituo mbalimbali vya kijeshi nchini Liberia bila ya kutokea ajali hata moja.

    Katika nchi za kigeni, usalama ni suala muhimu la kwanza kwa askari hao. Bw. Wang Qiu Sheng alisema kuwa, "Uendeshaji wa gari ulikabiliwa na hali ya hatari katika siku za kawaida. Nchini Liberia, tulikuwa tukikabiliwa na hali ya wasiwasi ya migogoro katika sehemu ngeni kwetu, hivyo tulipaswa kuangalia masuala ya usalama kila wakati, kama vile usalama wa askari, magari na wa vituo vyetu vya kijeshi. Ulinzi wa amani ni kazi yetu, vilevile ni jukumu letu kuhakikisha usalama wa askari.

    Hata hivyo, hali ya hatari ilitokea tarehe 4, Aprili. Siku hiyo kikundi cha ulinzi wa amani cha China kilipokea amri ya dharura. Kilipaswa kuchukua vifaa na baadhi ya askari wa kituo cha mwisho cha ulinzi wa amani wa Pakistan hadi Voinjama. Voinjama iko kwenye urefu wa mita 500 juu ya usawa wa bahari kwenye sehemu ya misitu ya kitrpiki nchini Liberia, ni moja kati ya sehemu zenye matatizo makubwa nchini humo. Ili kuhakikisha kazi hiyo inamalizika kwa wakati, naibu mkuu wa kikundi hicho Bw. Hong Dagang aliongoza magari 22 kutekeleza kazi hiyo. Wakati huo, nchini Liberia yalikuwa ni majira ya masika, mvua zilinyesha huku upepo mkali ukivuma, siku iliyofuata, magari yalikwama mara kwa mara kwenye matope na vinamasi. Lakini askari wa kikundi hicho walifanya juhudi kwa wawezavyo kuondoa matatizo yote na kuendelea na kazi ya uchukuzi. Usiku huo saa moja na dakika 40, wakati magari ya kikundi cha ulinzi cha China yalipowasili huko Volinjama, kamanda wa jeshi la Pakistan alitiwa moyo sana na kusema kwa furaha, "Magari ya nchi nyingine mbili hayakufika hapa kutokana na matatizo safarini, lakini jeshi la ulinzi wa amani la China limefanikiwa kumaliza kazi hiyo!" Kutokana na tukio hilo, jeshi la ulinzi wa amani la Pakistan liliandika barua ya shukurani kwa makao makuu ya Umoja wa Mataifa nchini Liberia, ili kushukuru misaada isiyo na uchoyo ya jeshi la ulinzi wa amni la China. Kwenye barua hiyo waliandika: Katika vituo vya ulinzi wa amani, kikundi cha uchukuzi cha China kilichobeba jukumu kubwa; katika jukwaa la kimataifa, China ni nchi inayowajibika jukumu kubwa!"

    Kutokana juhudi kubwa, katika mwaka uliopita, "China, OK" I;oweza kusikika mara kwa mara kila kilipopita kikundi cha usafirishaji cha China. Hii si kama tu ni sifa kwa askari wa jeshi la ulinzi wa China, bali pia ni kwa China inayopenda amani.

Idhaa ya Kiswahili 2005-02-11