Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-17 15:23:22    
Mchezaji hodari wa mpira wa mezani wa China Bi Deng Yaping

cri

Urefu wake ni mita 1.5 tu;

Amepata ubingwa wa dunia mara 18;

Yeye ni mchezaji hodari nchini China hata duniani;

Baada ya kuondoka kutoka kwenye timu ya China alikwenda kusoma katika Chuo Kikuu cha Qinghua

Alipata shahada ya pili katika chuo kikuu cha Nottingham;

Hivi sasa anajitahidi kupata shahada ya tatu katika Chuo kikuu cha Cambridge cha Uingreza;

Alitoa mchango mkubwa kwa Beijing kupatanafasi ya kuandaa mashindano ya Olimpiki ya mwaka 2008;

Yeye ni mchezaji wa mpira wa meza wa China Bi Deng Yaping

Bi Deng Yaping ni mchezaji hodari nchini China, si kama tu alipata medali nyingi za dhahabu, bali pia uchezaji wake wenye imani kubwa katika michezo ulipendwa na kuwavutia watu wa China. Ingawa ameondoka kutoka kwenye timu ya China, lakini hivi sasa katika maisha yake bado ana shughuli nyingi.

Mwaka 1997 baada ya kuondoka kwenye timu ya mchezo wa mpira wa meza ya China alianza kusoma katika chuo kikuu cha Qinghua cha China, akijifunza lugha ya kingereza. Katika miaka minne chuoni Bi Deng Yaping alifanya juhudi kubwa. Ingawa yeye alikuwa ni bingwa wa dunia, lakini katika masomo yake alikuwa anawaheshimu sana walimu na wanafunzi wenzake. Mwaka 2001, alikwenda Uingereza ili kujipatia shahada ya pili. Katika kipindi hicho, mara akirudi China aliwatembelea walimu wake waliomfundisha katika chuo kikuu cha Qinghua. Alisema kuwa, Qinghua ni nyumbani kwake na walimu ni wafamilia yake.

Katika chuo kikuu cha Nottingham anasoma "utafiti wa China ya kisasa". Kuhusu somo lake alisema kuwa, zamani rafiki zake wa kigeni walikuwa wakimwuliza kuwa, ni kwa nini wachezaji wa kike wa China walipata medali nyingi zaidi kuliko wachezaji wa kiume wa China? Mwanzoni hakufikiri suala hilo, lakini baadaye alipofikiri kwa makini alitambua kuwa jambo hili linastahili kufanyiwa utafiti wa makini. Hivyo alianza kuandika makala yake kuhusu taaluma ya "kuwa bingwa wa dunia", baada ya mwaka mmoja katika mtihani wa kuhitimu alitoa hotuba yake kuhusu mabadiliko makubwa ya wanawake wa China na michezo nchini China. Maofisa wote walimsifu sana kwa hotuba yake.

Mwaka 2003, Bi Deng Yaping alirudi China kutoka chuo kikuu cha Cambridge ambapo alikuwa amejipatia shahada ya pili, ili kufanya kazi katika Kamati ya Olimpiki ya mwaka 2008 ya Beijing. Kwa kuwa mwalimu wake wa Chuo kikuu cha Cambridge Bw. Peter Newlandni mtaalamu hodari wa uchumi, alikuwa ametafiti uchumi wa China miaka 30, alitambua kuwa, mashindano ya Olimpiki ya mwaka 2008 yataleta athari kubwa kwa uchumi wa China, hivyo aliona kuwa, kurudi China kwa Bi Deng Yaping, si kama tu kunamwezesha kulihudumia kuhuduma taifa lake, bali pia kutamwezesha kupata habari nyingi kwa ajili ya makala yake ya taaluma.

Kuhusu siku za usoni, Bi Deng Yaping alisema kuwa, China ilimwandaa kuwa bingwa wa dunia, anapaswa kusoma na kufanya kazi kwa bidii ili kutoa mchango kwa maendeleo ya michezo ya China.

Idhaa ya kiswahili 2005-02-17