Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-17 17:07:14    
Sikukuu za Kichina

cri

    Sikukuu ya Spring: Kila mwaka mwishoni mwa majira ya baridi ambapo majira ya Spring yanakaribia. Wachina husherehekea sikukuu ya kwanza katika mwaka mmoja, yaani sikukuu ya Spring(sikukuu ya jadi ya mwaka mpya wa Kichina). Katika sikukuu hiyo, familia nyingi hubandika mlangoni karatasi pacha zenye maneno ya baraka na picha katika nyumba zao. Kukesha wa kuamkia sikukuu ya Spring ni desturi ya Wachina, kwamba jamaa wote wa familia hukusanyika na kula chakula cha jioni pamoja kwa furaha hadi mapambazuko. Katika asubuhi ya siku ya pili, watu wote huenda kuwasalimu jamaa na marafiki zao, na kuwatakia heri na baraka katika mwaka mpya. Katika kipindi cha sikukuu ya Spring, sherehe za kijadi hufanyika katika sehemu mbalimbali.

    

    Sikuku ya taa: Tarehe 15 mwezi wa kwanza kwa kalenda ya Kichina ni sikukuu ya taa. Siku hiyo ni siku ya kwanza ya mwezi mpevu katika mwaka. Kuna desturi ya kula "yuanxiao" na kuburudikana maonesho ya taa za aina mbalimbali katika sikukuu hiyo. "Yuanxiao" ni vidonge duara vinavyotengenezwa kwa unga wa mchele wenye sukari ndani yake. Chakula hicho kukusanyika pamoja kwa jamaa wa familia. Desturi ya kutazama maonesho ya taa ilianza katika karne ya kwanza, mpaka sasa bado imevuma sana nchini China. Kila ifikapo usiku wa sikukuu hiyo, maonesho ya taa hufanyika katika miji mbalimbali na taa za kila aina huoneshwa.

    

    Sikukuu ya kusafisha makaburi: Tarehe 5 mwezi Aprili kila mwaka ni sikukuu ya kusafisha makaburi. Zamani sikukuu hiyo ilikuwa siku ya kuwafanyia tambiko mababu, hivi sasa katika siku hiyo watu hutembelea makaburi ya mashujaa na kuwakumbuka. Wakati huo hali ya hewa huwa ni ya fufutende, majani na miti huanza kuchipuka, hivyo watu hutembelea vitongojini kufurahia mwanzo wa spring na kurusha tiara, hivyo sikukuu hiyo pia inaitwa "sikukuu ya matembezi katika majira ya spring".

    

    Sikukuu ya mashua ya Dragoni: tarehe 5 mwezi wa tano kwa kalenda ya Kichina ni sikukuu ya mashua ya Dragoni. Inasemekana kuwa sikukuu hiyo ilianzishwa kwa ajili ya kumkumbuka mshairi mzalendo wa kale Qu Yuan. Qu Yuan alikuwa mtu wa dola la Chu katika Enzi ya Madola ya Kivita(475k.k.-221k.k.). alijitumukiza mtoni tarehe 5 mwezi wa tano mwaka 278 K.K. kutokana na dola la Chu kukaliwa na dola la Qin. Baadaye watu humkumbuka kwa kuendesha mashua yenye kichwa kinachofanana na dragoni. Chakula cha kijadi katika sikukuu hiyo kinaitwa "zongzi" ambacho ni chakula kinachotengenezwa kwa mchele uliofungwa kwenye na majani ya matete.

     

    Sikukuu ya mwezi: Tarehe 15 mwezi wa nane kwa kalenda ya Kichina ni sikukuu katikati ya majira ya Autumn. Katika zama za kale, watu walitumia kekiya mwezi kumwabudu mungu wa mwezi, baadaye jamaa wote walikula keki hiyo ya duara ambayo inafanana na mwezi mpevu katika sikuku hiyo. Jamaa wote hujiunga pamoja kwa furaha. Desturi hiyo inaendelea mpaka sasa.

     

Idhaa ya Kiswahili 2005-02-17