Wagonjwa wa Ukimwi Wakati virusi vinavyosababisha Ukimwi HIV vinapoongezeka hadi kiasi fulani mwilini, kinga ya mwili inafifia kiasi ambacho inashindwa kujikinga na bakteria, wakati huo inakuwa rahisi kwa binadamu kupata magonjwa ya aina nyingi kama kuhara tumbo, homa ya mapafu, saratani na au kuwa punguani, wakati huo mtu huyo anakuwa ni mgonjwa wa Ukimwi, mwishowe mgonjwa wa Ukimwi hufa kwa magonjwa hayo. Toka mtu anapoambukizwa virusi vya Ukimwi hadi kuwa mgonjwa wa Ukimwi kwa kipindi kifupi ni miezi kadhaa, kwa kirefu ni miaka kumi au hata kirefu zaidi, kwa wastani ni miaka 7 hadi 10.
|