Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-18 16:08:05    
AIDS (UKIMWI) 20

cri
Mawasiliano ya kawaida hayaambukizi Ukimwi

Utafiti wa aina nyingi umethibitisha kuwa mawasiliano ya kawaida na wagonjwa wa Ukimwi hayaambukizi ugonjwa wa Ukimwi.

Mawasiliano ya kawaida kama kushikana mikono, kukumbatiana, kubusiana kiadabu, kula pamoja, kutumia pamoja vyombo vya kazi za mikono na vya ofisini na noti, yote hayo hayaambukizi Ukimwi.

Kadhalika, Ukimwi hauambukizwi kwa kutumia pamoja na wagonjwa wa Ukimwi choo cha kukalia, simu, vyombo vya kulia, malazi, bwawa la kuogelea na vyombo vyovyote vya umma.

Kukohoa na kupiga chafya pia haviambukizi Ukimwi.

Aidha, mbu hawaambukizi Ukimwi. Utafiti umebaini kuwa virusi vya HIV havizaliani ndani ya mwili wa mbu. Mbu anapouma mtu haingizi damu yake ndani ya mwili wa mwanadamu bali aliingiza tu mate yake kwa ajili ya kurahisisha sindano yake kuingia kwenye mwili wa binadamu. Baada ya kufyonza damu ya mwanadamu mbu hatamwua mwingine mara moja bali atapumzika kwa muda ili ayeyushe damu ya mtu na kuwa lishe yake. Mpaka sasa hakuna habari yoyote duniani kuhusu mtu aliyeambukizwa Ukimwi kutokana na kuumwa na mbu.