Mji wa Xi Shuang Ban Na uliopo kwenye mkoa wa Yunnan nchini China ulipewa jina la "Maskani ya Yausi". Mtu akitazama chini kutoka juu, anaweza kuona vijiji zaidi ya 10 vilivyoko kwenye kingo mbili za Mto Lancang, vikiwa vimetawanyika huko na huko kama bombwe la tausi.
Yang Liping, bingwa wa kucheza ngoma wa kabila la Wabai alizaliwa na kuishi kwenye maskani hayo ya tausi. Alianza kucheza ngoma ya tausi kutokana na kuupenda, pamoja na wenzake kijijini tangu alipokuwa na umri wa miaka minne, wakati mwingine alipochoka kutokana na kucheza ngoma hiyo aliingia kwenye ghorofa ya mianzi na kulala fofofo.
Zaidi ya miaka 36 imekwishapita, Yang Liping amebadilika kutoka msichana mdogo na kuwa "tausi wa dhahabu" wa kweli katika uwanja wa ngoma wa China. Ngoma ya mchezaji mmoja "Roho ya Tausi" iliyotungwa na kuchezwa naye, ilipata tuzo ya daraja la kwanza ya utungaji katika Mashindano ya Pili ya Ngoma ya Taifa na pia ilipata ushindi wa kwanza katika uchezaji ngoma. Mwaka 1987 alialikwa kuwa Mwanachama wa Kudumu wa Jumuiya ya Ngoma za Kienyeji ya Taifa ya Philippines, hivi sasa amekuwa mchezaji anayejulikana katika uwanja wa sanaa.
Ngoma ya tausi inayochezwa na Yang Liping inapendwa na watazamaji wote. Mafanikio ya ngoma " Roho ya Tausi" yalimfanya awe na tumaini kubwa zaidi. Mwaka fulani alirudi mkoani Yunnan mara nne kukusanya nyimbo za kienyeji na kubuni ngoma 10 zenye mtindo wa makabila ya Wadai, Wayi, Wadong, Wava na Wajingpo na za makabila mengine mawili. Alicheza ngoma hizo katika tumbuizo moja. Katika majira ya Chipuko ya mwaka 1988 Yang Liping alizuru Philippini ambako alifanya matumbuizo ya ngoma. Maonesho hayo zilishangiliwa sana kwenye Mji wa Manila. Mwezi wa Juni, ngoma hizo yalioneshwa katika Mji wa Beijing, nayo yalifurahisha sana watazamaji. Yang Liping amekuwa bingwa mchezaji ngoma wa kwanza aliyefanya maonesho ya ngoma binafsi katika nchi ya nje na pia alikuwa msanii mwenye umri mdogo kabisa kufanya matumbuizo ya ngoma nchini China.
Ngoma za Yang Liping hazifuati kanuni za vyuo vikuu na za ngoma za kale, bali zina mtindo wa kipekee. Alipokuwa na umri wa miaka 12 bila ya kumwambia mama yake, Yang Liping alijiunga na Kikundi cha Michezo cha Xi Shuang Ban Na baada ya kufaulu mitihani. Ingawa mama yake alimtaka abaki nyumbani kuwasaidia ndugu zake wadogo na kumlazimisha aachane na kikundi hicho cha michezo, Yang alikataa kabisa na kulia sana kwani aliona kuwa ngoma ndiyo maisha yake.
Mwaka 1978 kwa mara ya kwanza Yang Liping aliigiza kama binti mfalme tausi katika ngoma moja. Kutokana na opera hiyo umahiri wake ulionekana wazi, kwa hiyo alihamishiwa kwenye Kikundi Kikuu cha Nyimbo na Ngoma za Makabila mjini Beijing.
Takriban watu wote wa kabila la Wadai wanajua kucheza ngoma ya tausi. Bingwa wa kwanza wa ngoma ya tausi wa China alikuwa msanii wa kienyeji Mao Xiang, wa pili alikuwa bingwa wa kabila la Wadai wa kucheza ngoma Dao Meilan. Uchezaji wa ngoma ya tausi umekwishafikia kiwango cha juu sana, si jambo rahisi kwa mtu yeyote kukipita kiwango hicho, lakini Yang Liping ana mtindo wake mzuri wa kipekee wa kuonyesha vizuri roho ya tausi, hivyo akawa bingwa wa tausi wa tatu.
Uchezaji ngoma wa Yang Liping unaonesha desturi maalumu ya Kikabila, pia mchezaji huyo ana mtindo wake mwenyewe na hutumia njia ya kisasa ya uchezaji. Anaona kuwa ni kutokana na kufanya hivyo tu ndipo anapoweza kutofautiana na wengine.
Wachambuzi wengi wanaona kuwa uchezaji ngoma wa Yang Liping una nguvu za ajabu zinazotokana na kipawa chake. Yang mwenyewe alisema kuwa licha ya kipawa chake pia huwa anacheza kwa moyo wote. Yang ana ushupavu mkubwa kuliko wenzake, ndiyo maana akapata mafanikio makubwa zaidi.
Picha Husika>>
1 2 3 4
|