Mji wa Harbin uko kaskazini mashariki mwa China. Mto Songhuajiang unapitia kwenye mji huo, na kuufanya mji huo uwe na mandhari nzuri zaidi na maliasili nyingi. Mji wa Harbin uko katikati ya Asia ya Kaskazini Magharibi, na unasifiwa kuwa ni moja ya lulu zilizopo kwenye daraja linalounganisha Ulaya na Asia. Reli tano kutoka kwenye mji huo hadi kufika kwenye miji ya mji wa Dalian, Suifenhe, Manzhouli, Bei'an na Lafa zimeunganisha miji nchini China na nje ya China, mto wa Songhuajiang unaweza kufikia nchini Russia moja kwa moja, na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Taiping unaweza kusafirisha kuabiria milioni 2 kwa mwaka.
Mji wa Harbin una mitaa minane na wilaya 11. Eneo la mji huo ni kilomita za mraba 53,068. Idadi ya watu wa mji huo ni milioni 9.543, kati yao watu milioni 3.84 ni wakazi wa mjini. Mji huo ni mji mkuu wa mkoa wa Heilongjiang na pia ni kituo cha kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni, sayansi na mawasiliano cha mkoa huo.
Mito mingi mjini Harbin ni ya mfumo wa Mto Songhuajiang na Mto Mudanjiang. Mjini humo mvua hunyesha katika kipindi cha mwezi Juni hadi mwezi Septemba. Kiasi cha rasilimali ya maji kwa kila mtu ni mita za uajzo 1363. Hali ya hewa huko ni ya pepo za msimu za aina ya barani ya ukanda wa fufutende. Majira ya baridi huwa ni marefu na majira ya joto huwa ni mafupi, hivyo mji huo pia unasifiwa kama ni mji wa barafu. Una maliasili nyingi ya madini, ambazo aina 83 za madini zimegunduliwa, na miongoni mwa madini hayo aina 25 zinaweza kutumiwa viwandani. Aina 20 za madini yakiwemo makaa ya mawe na gesi asilia ni madini muhimu sana ya mkoa wa Heilongjiang. Na maliasili ya mimea pia ni nyingi. Mimea ya dawa, mimea ya chakula na mimea ya mafuta yote ina thamani kubwa ya kiuchumi, na ni sehemu muhimu katika mauzo ya bidhaa katika nchi za nje. Aina na idadi ya wanyama pori pia ni nyingi. Kuna wanyama wengi muhimu wanaohifadhiwa na serikali kama vile chui wa kaskazini mashariki na korongo mweupe.
Mji wa Harbin una hisitoria ndefu, ambao ni chimbuko la Enzi ya Jin na Enzi ya Qing. Na mji huo ulipata maendeleo ya kasi baada ya ujenzi wa reli ya China Mashariki mwishoni mwa karne 19.
Baada ya China kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, mabadiliko makubwa yalitokea mjini Harbin. Uchumi na jamii imepata maendeleo makubwa. Mji huo umekuwa mji wa kisasa wenye viwanda vya aina mbalimbali na vijiji vingi.
Uamuzi wa kimkakati wa kufanya marekebisho katika vituo vikongwe vya viwanda vya kaskazini mashariki mwa China uliotolewa kwenye mkutano wa 3 wa kamati kuu ya 16 ya chama cha kikomunisti cha China, umeupatia mji wa Harbin fursa mkubwa ya maendeleo. Mji huo ulitunga mpango wa marekebisho ya kituo kikongwe cha viwanda mjini humo, na marekebisho yameanza kupata maendeleo. Miradi 590 imepangwa ambayo gharama ya uwekezaji imefikia yuan za renminbi bilioni 124. Na miongoni mwa miradi hiyo, miradi 17 imewekwa katika mpango wa kwanza wa taifa wa marekebisho ya kituo cha viwanda, na thamani ya uwekezaji wa miradi hiyo ni yuan za renminbi bilioni 2.67.
Picha husika
1 2
|