Mahitaji
Doufu gramu 300, tango moja, uyoga mweusi gramu 20, kisasi kidogo cha pilipili mbuzi na tangawizi
Njia
1. kata doufu na tango ziwe vipande vidogo, osha uyoga mweusi na kuikata vipande.
2. baada ya kuchemsha maji yenye chumvi, tia vipande vya doufu na uyoga mweusi ndani ya maji, chemsha tena, vipakue, na vipooze kwa maji baridi.
3. tia mafuta kidogo ndani ya sufuria, mpaka yachemke, tia pilipili kima baada ya pilipili mbuzi kuwa nyeusi ipakue, tia vipande vya tangawizi ndani ya mafuta hayo.
4. mimina mafuta hayo kwenye vipande vya doufu na uyoga mweusi, tia chumvi na M.S.G, korogakoroga. Kitoweo hiki sasa kiko tayari.
|