Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-11 21:42:27    
Wagonjwa wa Ukimwi watibiwe nyumbani

cri

Idara ya Afya ya mji wa Zhuizhou yachukua hatua za kuzuia maambukizi ya Ukimwi kutoka kwa wazazi kwenda kwa watoto

   Hivi karibuni idara ya afya ya mji wa Zhengzhou imechukua hatua za kuzuia maambukizi ya Ukimwi kutoka kwa wazazi kwenda kwa watoto. Madaktari wa vijijini, zahanati za tarafa na hospitali za ngazi ya wilaya na vituo vya udhibiti wa maambukizi ya magonjwa vinapewa majukumu tofauti kwa ajili ya kuweka "vizuizi" vinne vya kukatisha njia ya kuambukiza mtoto ugonjwa wa Ukimwi.

   Kutokana na hatua zilizowekwa, madaktari wa vijijini wanawajibika kuwapatia wajawazito elimu ya afya na ujuzi wa Ukimwi, na kufuatilia hali za wajawazito wenye virusi vya Ukimwi. Na watoto waliozaliwa na wagonjwa wa Ukimwi wanafuatiliwa hali yao na kuwaelekeza wazazi namna ya kuwalisha; Zahanati za tarafa zinawajibika kuwaelekeza na kuwasaidia kikazi madaktari wa vijijini; idara za afya na hospitali za ngazi za wilaya zinazoshughulikia huduma za ukunga na afya kabla ya ndoa zinawajibika kutoa elimu ya afya ya kabla ya ndoa; vituo a udhibiti wa maambukizi ya magonjwa vinawajibika kuandaa watu, kusimamia dawa na kukusanya taarifa.

   Mkuu wa Idara ya Afya ya mji wa Zhengzhou aliwaambia waandishi wa habari kwamba kwa kawaida, ugonjwa wa Ukimwi unaambukizwa kwa njia ya damu, ngono na wagonjwa wajawazito. Ili kuzuia maambukizi kwa njia mbili za mwanzo, idara za afya zimeanza kufanya ukaguzi mjini kote kuhusu shughuli za kuchangia damu  na kushawishi watu kutumia kondomu.

Idhaa ya Kiswahili 2005-03-11


1  2