Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-11 21:52:10    
Zhang Cunsheng na Udongo wa Chengni

cri

    Miaka mitano iliyopita Zhang Cunsheng aliuona Mto Manjano kwa mara ya kwanza, mto huo mrefu na mpana na mila mbalimbali za wakazi walioishi kando yake vilimsisimua sana msanii huyo wa jadi wa mkoa wa Anhui na kuamaua kubakia mkoani Henan ambako aliishi kwenye nyumba iliyokuwa kando kando ya mto huo. Mchana alikwenda kando ya mto na kubeba gunia moja baada ya jingine la udongo wa mtoni, na kuutumia udongo huo kutengeneza vinyago vya udongo vya namna kwa namna kama vile vyombo vya kuwekea brashi, sanaa za kutundikma kutani, mawe ya wino (inkstone) au vichwa vya wanyawa. Usiku alikuwa akinoa vinyago hivyo au kuchonga nakshi juu yao, baadaye kuyatia ndani ya moto mkali kuyachoma na kuyaoka, baada ya kuyatoa kutoka kwenye tanuni alikuwa akiyatia ndani ya karai na kuyapika kwa kutumia mvuke pamoja na nta nyeusi, siki na miti-shamba, mwishowe alikuwa anapata vitu vya sanaa vyenye mvuto mkubwa. Kwa kutumia akili zake na mikono yake Zhang Cunsheng alizusha upya sanaa ya "Matope ya Chengni" iliyoacha kupokezanwa kwa muda wa makumi ya miaka. Sanaa ya "Udongo wa Chengni ni ustadi wa jadi wenye historia ndefu kwenye eneo la Zhongyuan (sehemu ya katikati ya China).

    "Mawe ya wino ya udongo wa Chengni" yaliyotengeneza kwa njia hiyo yaliwahi kudhaniwa kuwa ni mawe mazuri na bora kabisa ya wino nchini China mnamo Enzi ya Tang. Zhang Cunsheng alichanganya sanaa ya kale iliyoanzishwa enzi hiyo na maumbo na dhana za kisasa. Vitu alivyotengeneza kwa kutumia udongo wa Chengni havikurithi hulka za kijadi tu, bali pia vilichanganya baadhi ya vitu vya kisasa na vya kidhaniwa. Mawe ya wino aliyotengeneza kwa udongo wa Chengni ni bora na imara, nje yake ni laini, lakini si ya kuteleza, isitoshe huwa na rangi za kijani, nyekundu, manjano, kijivu na kahawia zilizopatikana baada ya kuchomwa. Vitu hivyo vingi vimehifadhiwa kwenye majumba ya makumbusho. Mapambo ya kutundika kutani na vitu vya kuigiza vyombo vya kale alivyovitengeneza, huwapa watu hisia ya kuwa vina nguvu za kimaumbile. Tukieleza kwa kuazima maneno ya Zhang Cunsheng mwenyewe ni kuwa udongo wa huko, mila za wakazi wa huko na Mto Manjano vilimpa msisimko na nguvu za kutengenezea sanaa hizo. Kutokana na kutegemea nguvu hizo pamoja na nia yake, Zhang alimaliza "Safari ya Kuelekea Magharibi", michongo kabambe ya matofali ambayo jumla ya urefu wa seti hiyo ni mita 30, na ilitumia miaka mitatu. Sanamu 2,000 za binadamu, mashetani, wanyama, milima, maporomoko ya maji na miti zilipangwa pamoja kwa ustadi na werevu, nazo huwapa watazamaji hisia ya uhalisi wa kuweko katika maumbile.

Idhaa ya Kiswahili 2005-03-11