Mahitaji
Nyama ya nguruwe gramu 240, chumvi gramu 2, pilipili manga gramu 2, mvinyo wa manjano gramu 10, uyoga gramu 20, mchuzi wa nyanya vijiko 2, kitunguu saumu 1, kiasi kidogo cha kitunguu, pilipili mboga moja, sukari na mafuta
Njia
1. Kata sarara ya nyama ya nguruwe iwe vipande vyembamba na ipakue ndani ya bakuli moja, tia chumvi, pilipili manga na mvinyo wa manjano. Kata kitunguu, uyoga na kitunguu saumu vipande vipande.
2. tia mafuta ndani ya sufuria, pasha moto mpaka yawe na joto la nyuzi kati ya 50 na 60, tia vipande vya sarara na vikaange mpaka viwe na rangi ya hudhurungi, kisha vipakue.
3. pasha moto tena, tia vipande vya kitunguu na kitunguu saumu, korogakoroga, tia uyoga, koroga, tia mchuzi wa nyanya, tia sukari na mimina maji, chemsha, tia pilipili mboga, ongeza moto na ukoroge.
4. tia vipande vya sarara vilivyokaangwa na koroga, tia chumvi na pilipili manga. Mpaka hapo kitoweo hiki kitakuwa tayari, kipakue tayari kuliwa.
|