Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu ukimwi ulifanyika leo hapa Beijing, naibu waziri mkuu wa China bibi Wu Yi alipotoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano alisema kuwa, serikali ya China inazingatia sana udhibiti wa ukimwi.
Bibi Wu Yi alisema kuwa ukimwi umetia changamoto kali kwa maisha na maendeleo ya binadamu na umekuwa suala kubwa linalohusu afya za watu na jamii. Amesema serikali ya china itaboresha sheria na kanuni husika, kutenga fedha nyingi zaidi na kutekeleza sera husika.
Mkutano huo unaendeshwa kwa pamoja na Shirikisho la Kampuni Duniani dhidi ya ukimwi na wizara ya afya ya China, wawakilishi karibu 400 kutoka kampuni za China na Marekani pamoja na baadhi ya jumuiya duniani walishiriki kwenye mkutano huo.
|