Mahitaji
Uyoga mweusi gramu 10, pilipili mboga gramu 5, pilipili nyekundu gramu 5, nanasi, yai moja, kiasi kidogo cha mchuzi wa soya, chumvi, kitunguu maji, wali uliopikwa na mafuta
Njia
1. Kata uyoga mweusi, pilipili mboga na pilipili nyekundu na nanasi ziwe vipande vidogo. Koroga yai.
2. tia mafuta ndani ya sufuria, mpaka yachemke, tia vipande vya kitunguu maji, halafu tia vipande vya uyoga mweusi, pilipili mboga na pilipili nyekundu na nanasi na korogakoroga, zipakue.
3. pasha moto tena, tia mafuta kidogo na mimina yai na tia wali, koroga koroga, halafu tia vipande vya uyoga mweusi, pilipili mboga na pilipili nyekundu na nanasi, koroga, mimina mchuzi wa soya na chumvi, koroga ichemke kidogo. Mpaka hapo, mseto uko tayari kuliwa
|